Kwa ukaribu huu wa Wema na Diamond kulimfanya Dogo wetu Moses Iyobo kupata bahati ya mtende kilaini kwa dada yetu Aunt Ezekiel ambaye walianza mapenzi chini chini na kuficha kila walipoulizwa kama wana uhusiano ila alikataa, ila mwisho ya yote yalikuja julikana baada ya Aunt Ezekiel kupata ujauzito.
Sasa ikawa hawana jinsi lazima waweke wazi. Hatujui kama Madame Wema au Diamond alitumika kupiga pande kwa hawa wapenzi wawili ama la ila chanzo ni yeye kuwa na ukaribu na Diamond na Aunt Ezekiel ndo kukampa mwanya Moses Iyobo nae kuwa na uhusiano na Aunt Ezekiel.
Sasa leo kuna kamtihani kamemkuta Aunt Ezekiel kwa kuwa Madame Wema ameachana na Diamond Platinumz, na kuachana kwao kumetengeneza mgongano mpaka kupelekea kuwa na Team Diamond& Zari na Team Wema. Kwa kuangalia kwa umakini zaidi Aunt Ezekiel anakaribia kupata mtoto na Moses Iyobo na Upande mwingine bado yuko na Uswahiba na Wema Sepetu.
Aunt Ezekiel anapata mtihani kwa kulazimishwa na Wema kuwa bado awe kwenye Team Wema wakati yeye tayari ana usiano na Moses Iyobo ambaye ni Dancer wa Diamond na ukiangalia kwa umakini kila itakavyokuwa lazima Moses ndo anauhusika na kila kitu kwa huduma za Aunt Ezekiel.
Sasa ukiangalia kwa mbali kuna ugomvi wa chini chini kati ya Wema na Aunt Ezekiel ikisemekana kama Wema hataki Aunt Ezekiel amsapoti Diamond ila naamini Aunt Ezekiel anafanya ivi kwa mapenzi ya mpenzi wake Moses Iyobo.
Ukiwa kama wewe mdau unaweza mshauri nini Aunt Ezekiel;
1- Aaache kumsaport Diamond kwa kulinda urafiki wake na Wema?
2- Aache kumsaport Wema ali ajenge uhusiano zaidi na Moses Iyobo na kwa faida ya mtoto wao?
3- Au afanya uamuzi gani kwa hawa wahasimu wawili ili aweke mambo sawa kwa pande zote mbili.
Tumshauri dada yetu please bila matusi.
By Abatmwe on JF
Post a Comment