Msanii huyo amekiri kupitia eNewz kuwa, ni kweli yupo katika tishio la maisha yake, mhusika mkubwa wa hilo akiwa mwanaume ambaye alikuwa na mahusiano yake wa zamani ambaye hawana maelewano mazuri naye.
Wastara amesema kuwa, amekuwa na historia ya mahusiano mabovu na mtu huyo na kupelekea kuachana naye, na kitendo cha yeye kuolewa na marehemu Sajuki kikiwa sababu ya kuamsha ugomvi upya, na hapa anaeleza mwenyewe mambo yalivyoanza na kujikuta katika hali hiyo na vilevile hatua alizochukua, Wastara.
Wastara amesema kuwa, mwanaume huyo amekwishamtamkia wazi kuwa anahusika na moja ya ajali iliyomkumba, akitumia mambo ambayo ameyaita ya kiswahili kutaka kumuangamiza, jambo ambalo amekwishalitolea ripoti polisi takriban miaka 5 iliyopita.
Staa huyo amesema kuwa, chochote ambacho kitampata kwa mujibu wa maelezo aliyotoa kwa mwanausalama kutokana na vitisho vya bwana huyo, moja kwa moja vitakuwa vimemuweka hatiani, akisisitiza kuwa ana imani kuwa maisha yake yanasonga kwa mipango ya Mungu ambayo mwanadamu hawezi kuvuruga.
Post a Comment