Balozi
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, akifurahia jambo, wakati
akizungumza kwenye semina ya siku moja iliyoan daliwa na Mfuko huo kwa
kushirikiana naye, maalum kwa wanamitindo na wabunifu mavazi na
kufanhyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Jumapili Mei
Flaviana
(kulia) na Zuli Remtula,(katikati), mwanamitindo mwingine nguli
nzhini,na washiriki wengine wa semina hiyo, wakifuatilia maelezo
yaliyokuwa yakitolewa na Afisa wa PSPF, Magira Werema.
Wanamitindo
wakiwa kwenye foleni ya kupiga picha tayari kujipatia vitambulisho
baada ya kukamilisha zoezi la kujaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS
wa Mfuko huo.
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akizungumza jambo
na wenzake, Magira Werema, (kushoto), na Colleta Mnyamani, ambaye ni
Afisa Uhusiano wa Mfuko huo.
Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magira Werema, akitoa maelezo ya
kina kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na Mfguko huo
Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ambaye ni
Mwanamitindo na Mbunifu Mavazi maarufu nchini Tanzania, kwa sasa
akifanyia kazi zake nchini Marekani, akizungumza wakati wa semina ya
siku moja, iliyowaleta pamoja, wanamitindo "kinda" wa Tanzania, kwenye
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Jumapili Mei 17, 2015. Semina hiyo
ililenga kuwafunza na kubadilishana uzoefu juu ya tasnia hiyo inayokuwa
kwa kasi. Semina hiyo ya siku moja, ilitayarishwa kwa pamoja na Mfuko
wa Pensheni wa PSPF, na mwanamitindo huyo nguli. Katika maelezo yake,
Flaviana, alisema yeye binafsi ni mwanachama wa Mfuko huo kupitia
mpango wa hiari yaani "PSPF Supplementary Scheme-kwa kifupi PSS", na
kuwataka wanamitindo waliohudhuria semina hiyo, kufuata nyayo zake.
Aliwaeleza umuhimu wa wanamitindo hao ambao wengi ni vijana, kujiunga na
mpango huo kwa faida yao ya sasa na baadaye, kwani yeye anafaidika sana
kuwa mwanachama wa Mfuko huo. Baada ya maelezo hayo yaliyofuatiwa na
balozi mwingine wa Mfuko huo, Msanii maarufu wa muziki wa majigambo,
Mrisho Mpoto, naye aliwapa "doze" wanamitindo hao juu ya ukuhimu wa wao
kuchangamkia fursa mapema kwani ndio mtindo wa kisasa. Hali kadhalika
afisa masoko wa Mfuko huo Magira Werema, aliwahakikishia wanamitindo hao
kuwa Mfuko huo ni Mfuko bora na wala hawatajuta waingiapo kuwa
wanachama. Baada ya hotuba hizo, wanamitindo hao walizichangamkia fomu
za kujiunga na uanachama wa Mfuko huo amba;po karibu washiriki wote
zaidi ya 100 walijiunga na Mfuko huo.
Post a Comment