Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, ambae pia ni mgombea urais kupitia Chama cha Chadema.
Dar es Salaam. Polisi mjini
Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais kupitia
Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria mazishi ya
kada wa CCM, Peter Kisumo.
Vyanzo vya kuaminika
toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara huo kutokana na
kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi wa Ukawa na
wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi hawakuafiki.
Taarifa
zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi lilizusha
mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende mazishini
peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee yalikotoka
jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.
Baada ya
polisi kusisitiza kutoruhusu msafara mzima uende mazishini mgombea huyo
aliamua yeye na maofisa wengine alioambatana nao kurudi Mwanga
akisisitiza asingeweza kwenda peke yake akiwaacha watu aliambatana nao.
Source; (http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Msafara-wa-Lowassa-wazuiwa-kumzika-Kisumo/-/1597296/2831470/-/hv33aj/-/index.html)
Source; (http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Msafara-wa-Lowassa-wazuiwa-kumzika-Kisumo/-/1597296/2831470/-/hv33aj/-/index.html)
Post a Comment