Imelda mtema
Maskini Kajala! Ndivyo unavyoweza kusema ukisikia mkasa wa
staa wa kiwango cha juu kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Kajala
Masanja ‘Kay’, ambaye anadaiwa kwa hivi sasa hayuko sawa kiafya baada ya
kupigwa chupa kichwani akiwa katika shoo ya kumchangia mke wa msanii
Mabeste iliyofanyika New Maisha Club, Masaki jijini Dar.
Kajala Masanja akionekana na jeraha usoni kipindi ambacho alikua amepigwa chupa.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala kimeliambia Ijumaa Wikienda
kwamba, tangu staa huyo akumbwe na sekeseke hilo amekuwa katika kipindi
kigumu kwani amekuwa akipata maumivu makali sehemu ya kichwani huku
akianguka mara kwa mara.
Kajala Masanja.
Kilidai kwamba, pia Kajala amekuwa akipata kizunguzungu kikali hivyo
kujiona yupo kwenye hatari kubwa hasa ikitokea akaanguka vibaya kwani
anaweza kupoteza maisha.
ASHINDWA KUENDESHA GARI
Mpashaji wetu huyo aliweka wazi kuwa tangu Kajala akumbane na mkasa
huo mzito uliomsababishia kushonwa nyuzi mbili juu ya jicho, amekuwa
hayuko vizuri na kuna wakati hawezi hata kuendesha gari hivyo kukwamisha
shughuli zake za kila siku.
“Kiukweli Kajala hayupo vizuri kabisa, amekuwa kwenye kipindi kigumu mno tangu alipopigwa chupa klabu.
“Amekuwa akianguka mara kwa mara kutokana na kizunguzungu kikali anachopata akisimama au kutembea,” kilisema chanzo hicho.
CT-SCAN;mfano wa mashine ambayo Kajala amefanyiwa vipimo.
ATINGA HOSPITALINI
Habari zilizidi kumiminika kuwa, baada ya kuona hivyo Kajala
alikwenda kwenye Hospitali ya Regency iliyopo Upanga jijini Dar kwa
ajili ya kufanya vipimo.
AFANYIWA CT-SCAN
Kilisema kuwa alipofika hospitalini hapo alifanyiwa kipimo cha
CT-SCAN kichwani ambapo majibu yalipotoka aliambiwa kuwa kinachomsumbua
ni damu iliyoganda sehemu aliyopigwa chupa.
MAJIBU YA DAKTARI
“Daktari alimpa majibu ya kushangaza maana alimwambia kama
angezembea, tatizo lingekuwa kubwa sana kwenye ubongo na lingeleta shida
zaidi,” kilisema chanzo hicho.
HUYU HAPA KAJALA
Baada ya kunyetishiwa mkasa huo wa kusikitisha, Ijumaa Wikienda
lilimtafuta Kajala ili kuthibitisha tatizo hilo alilokuwa nalo ambapo
alikiri kuwa alikuwa akihisi kizunguzungu kikali cha mara kwa mara
lakini hakuwa amegundua kama alikuwa na tatizo la kuvilia damu kichwani.
“Lakini kwa sasa namshukuru Mungu niko sawa kidogo. Ukweli nilikuwa
napata shida sana kila nikiinuka, napata shida ya kizunguzungu kikali
sana,” alisema Kajala.
TUJIKUMBUSHE TUKIO
Wakati Kajala akitoka Klabu ya New Maisha hivi karibuni, akiwa
anashuka kwenye ngazi, ghafla alishangaa kurushiwa chupa kichwani
iliyosababisha kuanguka kutoka kwenye ngazi hadi chini na kusaidiwa na
wasamaria wema waliompeleka katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar
ambapo alishonwa jeraha alilolipata.
Katika sakata hilo, Kajala alisema kuwa mtu aliyempiga chupa ni
mwanaume na tayari yupo mikononi mwa polisi japo kabla ya tukio hilo
alikuwa hamjui na wala alikuwa hajawahi kumuona.....
Post a Comment