Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Nape Amchonoa Tena Lowassa........Asema CCM Iweza Kuyazuia MAFURIKO Kwa Mikono


Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejigamba kwamba kimeweza kuzuia ‘mafuriko’ kwa mikono huku kikiwatakia  kila la kheri baadhi ya makada wake waliotangaza kutogombea kupitia chama hicho pamoja na wale waliokihama na wanaotaka kukihama.

Mwishoni mwa wiki iliyopita waliokuwa madiwani jimbo la Monduli kupitia CCM mkoani Arusha, walitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku wabunge wa viti maalum, Ester Bulaya na James Lembeli aliyekuwa Mbunge wa Kahama wakitangaza kutogombea kupitia chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na mtandao huu  jana alisema CCM hakina uwezo wa kuzuia mtu anayetaka kukihama kwa sababu hiyo ndiyo demokrasia.

Aidha, Nape alisema vyombo vya habari vilimnukuu aliyekuwa mgombea urais kupitia CCM, Edward Lowassa akisema kuwa watu hawawezi kuzuia ‘mafuriko’ kwa mikono na kwamba CCM imeweza kufanya hivyo, lakini habari hizo haziandikwi.

Alisema wanachama wanaotaka kuhama hawawezi kuzuiwa kwa namna yoyote na kwamba hilo ni jambo la kawaida kufanyika kwa kada yoyote.

Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea urais, ulivyokuwa ndani ya CCM, alisema ulifuata utaratibu na kanuni zote na kwamba kama maneno mengi yataendelea kusemwa atatoa video inayoonyesha kila kitu kilivyokuwa ndani ya kikao cha Kamati Kuu (CC).

Kuhusu makada waliokihama chama hicho na kujiunga na Chadema, Nnauye alisema baada ya Baraza la Madiwani kuvunjwa hapakuwa tena na wawakilishi wa aina hiyo.

Alisema watu waliojiunga na Chadema huko Monduli mkoani Arusha hawakuwa Madiwani kwa kuwa Baraza la Madiwani likishavunjwa hakuna tena nafasi hizo za uwakilishi.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top