“Tumekabidhiwa orodha ya shughuli za leo.. kimsingi imekiuka kanuni, uamuzi wa kuileta hii miswada mitatu kwa pamoja kama hati ya dharura umekiuka kabisa msingi wa makubaliano ya kwenye Semina ambapo Wabunge kwa kauli moja tulikataa Miswada hii isiletwe kwa hati ya dharura“
“Naomba Mwongozo, hili jambo linahitaji majibu sasa” >>> Mbunge John Mnyika.
Spika Makinda akaanza kutoa ufafanuzi kuhusu hiyo ishu >>> “Toa kwanza maneno ya kuniamrisha mimi cha kufanya… Hakuna mtu anayeweza kuniamrisha” >>> Anne Makinda.
Spika akaendelea >>> “Tumefanya mara nyingi sana wala sio leo tu, hakuna kanuni iliyovunjwa na sio mara ya kwanza kujadili kitu kinachofanana kwa pamoja”>>> Spika Anne Makinda.
Hakukuwa na suluhu ya hilo, Wabunge wa Upinzani wakagomea Mjadala huo kuendelea ikabidi Kikao cha Bunge kiahirishwe saa nne asubuhi. Angalia Video Hapa:
Post a Comment