Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Wema Sepetu Awavua Nguo Nuh Na Shilole..Baada ya Wao Kudai Sauti ya Nuhu Akimtongoza Wema si ya Nuhu Bali Wema Ametengeneza Kuwagombanisha

Lile sakata la mrembo Wema Sepetu kutakwa kimapenzi na mpenzi wa msanii mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Nuh Mziwanda limeendelea kushika kasi ambapo Wema ameibuka na kuwavua nguo kwa kuwatolea maneno ya shombo.

Wema alitoa maneno hayo hivi karibuni baada ya Shilole na Nuh kumgeuka na kusema kwamba aliwachezea mchezo mchafu ili kuwagombanisha kwa sababu anawaona wanapendana hivyo alimtafuta mtu ambaye anaendana na sauti ya Nuh ili tu amharibie.

“Sijui kwa nini Wema kanifanyia hivi najua anataka tu kunigombanisha na mpenzi wangu kwa sababu hata ukisikiliza hiyo rekodi utasikia sauti ya Mirror akizungumza, hapo ndiyo ujue kuna mchezo mchafu sana na kwa hilo amefanikiwa lakini sisi huku mapenzi yetu yanaendelea,” alisema Nuh.

Kutokana na maneno hayo Wema alicharuka na kusema kwamba hawezi kutoa rekodi ya uongo na kumsingizia Nuh kwani ni mpuuzi na hawezi kujilinganisha naye kutokana na kwamba ni staa mkubwa.

“Nuh alinipigia na kunitaka kimapenzi ndipo nikaamua kumrekodi na hiyo ni sauti yake haijatengenezwa kama wao wanavyodai, kwanza nawashangaa hivi ningetengeneza sauti feki ili iweje, Nuh na Shilole siyo levo yangu ni wasanii wachanga sana, mimi ni staa mkubwa Tanzania na hakuna wa kulinganishwa na mimi labda nje ya Bongo.

"Nitafute kiki kwa kina Shilole  na Nuh kweli? Si bora nitengeneze kiki kwa kina Davido na wasanii wengine wakubwa duniani, hao si levo yangu jamani,” alisema Wema kwa sauti ya hasira.

Kabla ya kupatana, Nuh na Shilole waligombana hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni baada ya mrembo huyo kupokea sauti hiyo iliyosikika Nuh akimtongoza Wema.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

1 comments:

Halaf kajamaa kanakataa wakati huwa kana neno lake kanapenda kulitamka na hata kuliandika mara nyingi sana kanapokuwa na jambo lililomkera. Ndo kenyewe bhana kalitaka kusafirishwa na nyota ya wema tu alaah

Reply

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top