Nuh akiibusu pete ya uchumba aliyomvalisha Shilole
Ikimaanisha kuwa vita hiyo imetafsiriwa kama maandalizi ya kuachia ngoma mpya huku wengine wakiamini kuwa huenda ukawa ndio mwisho wa penzi lao.
Wakati wengine wakisheherekea sikukuu ya Eid weekend iliyoisha, Muimbaji wa ‘Nakomaa na Jiji’ Shilole alitumia akaunti yake ya Instagram kuandika vijembe kwa Nuh Mziwanda, alianza kwa kuandika:
“Mwanaume hata umfanyie nini haridhik lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakin mh! Nimejitahid nimehangaika’ila sasa kama gari limewaka’aka babu weeee kanikuta na maisha yangu wacha niendelee na maisha yangu’Mimi na yeye baaaaaaasi #GaNdALaNdiZi”
Baada ya siku moja Shishi aliongeza kijembe kingine:
“Kidume unataka raha tu ‘pesa hauna ‘na bado siunaleta ujanja kwa mtoto wa igunga ‘mjini hapa ‘halafu sina habari ‘wacha niwe busy na kazi zangu tu’mapenzi yashanishinda mie.nawapenda sana mashabiki wangu! Manopenda mitelemko kazi mnayo kupandisha vitonga hamtaki mtanyoookaa na kama ulikuwa unatembelea Kik yangu basi katafute snare”.
Upande wa Nuh Mziwanda naye alijibu kupitia akaunti yake:
“Mwanaume wa kweli ukaa kimya’sibishani na upumbavu’mwanamke asieridhika na kujua kua kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa’na kuvumilia mambo yote alionifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu’familia na’wasanii wenzangu na wadau’anaanza kunitukana mitandaoni for whaaaat!!! Mxeeeeew’mimi bado kijana na nna time ya kupata maisha yangu na mtu atakae thamini moyo wangu ‘nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari ‘mimi nacheka tu #AsHaNgeDerE”
Kama ni ‘kiki’ ya wimbo wao mpya, unahisi hashtag walizotumia #GaNdALaNdiZi na #AsHaNgeDerE zikawa zinahusika na jina la wimbo? Ngoja tusubiri tuone!
Post a Comment