Imelda Mtema
Muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Flava, Tunda Sabasita amejitapa kumpora bwana muuza nyago mwenzie, Agness Gerald ‘Masogange’ na kusababisha wawili hao kuingia kwenye bifu zito.Sosi aliye karibu na wauza nyago hao alisema kuwa bifu walilonalo linamhusu bwana aliyetajwa kwa jina moja la Said ambaye makazi yake ni nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’.
“Said ndiye aliyekuwa akimpa ‘good time’ Masogange alipokuwa Sauzi ambapo alikuwa akiishi maisha mazuri na baada ya kutibuana mwanaume huyo alihamishia majeshi kwa Tunda, kitendo kilichomuumiza Masogange ambaye walianza kurushiana matusi mtandaoni,” alisema sosi huyo.
Baada ya habari hiyo kutua kwenye Dawati la Ijumaa, mwandishi wetu alimsaka Masogange ambaye alikuwa mkali na kusema kuwa yeye hamfahamu Tunda wala hapendi kusikia habari hizo.
Muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Flava, Agness Gerald ‘Masogange’. “Kwanza simjui huyo Tunda wala sitaki kujua habari zake hata kidogo, naomba mniache,” alisema Masogange.
Tunda aliposomewa mashtaka yake alikiri kugombana na Masogange na kusema mwanaume huyo alipomfuata alimwambia walishaachana na Masogange hivyo yeye hana kosa.
“Said aliniambia wala sikujua kama alikuwa na Masogange, alisema walishaachana hivyo atulize presha hakuna sababu ya kuwapa watu faida,” alisema Tunda.
Post a Comment