Wema Sepetu...Si unajua kuna kundi la watu wengi nyuma yako??? Najua picha nyingi unazushiwa kuwa kimahusiano na hao watu mwisho wa siku inakuwa ni kwa ajili ya kazi. Iwe ni kweli au uongo....UNAPITILIZA... ni kama vile unatuambia niangalieni au semeni msemayo niko busy natengeneza pesa....ni sawa kimtazamo wako na jinsi ulivyo.
Lakini kuna siku ulisema unachukia matusi au umechoka watu kukuongelea na yote mpaka watu wanaitukana familia yako....huwezi kufikiria why?? Why unakasirika??? Na matusi yale yote...Ni kwa kuruhusu hasa picha kama hizi either kwa makusudi au bahati mbaya wale wenye nia mbaya na wewe wanatumia kama chambo kukudhalilisha wewe na familia yako..... Ukisearch kwenye internet za aina hiyo zinatokea nyingi mpaka watu huamini ni kweli wewe ni mchafu kitu ambacho si kweli, hali hii Unaweza kukosa opportunity kubwa sana kwenye nchi nyingine sababu ya yale ambayo unaona ni sawa kwako!
Ukikasirika ni poa tu lkn nakwambia picha zako kama ni za kibiashara usichukue muda mrefu kabla biashara haijawekwa wazi la sivyo hata sisi tumechoka kukataza watu waache kutukana wakati wewe mwenyewe unaona poa tu, wengine hutumia hayo kuanzisha teams za kukutukana!! .
.
Ukweli ni kwamba wale wanaokupenda kwa dhati wanazidiwa nguvu na wale wenye lengo la kukuharibia....na hao wenye nia ya kweli na wewe hukaa pemben hawana ujasiri wa kusema lolote sababu wanaogopa.....Naomba Useme kitu kwa wanaokupenda, ili ijulikane atakayekiuka basi ni wale wengine waharibifu ambao ni wengi kwa sasa. Tunakupenda lkn kuna mambo mengine si ya kufumbia macho wkt wewe mwenyewe unaweza kufanya kitu, fikiria cha kufanya au kama huwezi potezea!!!
By Mrekebishatabia
Post a Comment