Mwanasiasa Edward Ngoyai Lowassa ambaye yupo katika sintofamamu na chama chake CCM atazungumza na waandishi wa habari leo au kesho nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam iwapo atawahi kumaliza kikao na familia yake.
Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa mtoto wa Lowassa Fredy Lowassa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zake za kuelekea Urais kwa tiketi ya CCM zinaarifu kuwa Lowassa alianza kwa kufanya mazungumzo ya kina na familia yake huku katika kikao hicho Watoto wake wote wakihudhuria lakini pia wakwe zake akiwemo Sioi Sumari na kukubaliana baadhi ya mambo.
Mambo yanayodaiwa kukubaliwa na wanafamilia hao ni kwamba wawe tayari kumfuata katika chama chochote atakachoamua kuelekea, huku akishindwa kubainisha ni wapi atakapoelekea kwani alisisitiza kuwa hawezi kuhama au kutangaza uamuzi wowote pasipo kushauriana na marafiki zake wa karibu.
Hivi sasa waandishi wa habari wamefika nyumbani kwake Masaki hata hivyo wameombwa kuondoka na kuwa na subira kwani Lowassa bado anafanya mazungumzo na marafiki zake muhimu. mashuhuda kutoka eneo la tukio wanadai moja kati ya magari ya watu waliopo Nyumbani kwa Lowassa yameonekana kuwa ni yavmwenyekiti wa ccm wanawake taifa Sophia Simba, Lawrance Kago Masha, Adam Kimbisa, Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa vijana taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge zanzibar Sadifa Khamis, Hussein Bashe, Absolomon Kibanda, Khamis Mgeja(mwenyekiti ccm Shinyanga) Msukuma(mwenyekiti ccm Geita), Na Mgana Msindai(mwenyekiti CCM Singida).
===================
UPDATE: 12:40hours
Lowassa kaahirisha kuongea hadi taarifa zaidi itakapotolewa.
Taarifa iliyotumwa kwa wahariri leo asubuhi ilikuwa inasema:
Habari za asubuhi wahariri, Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa ana Press Conference
leo Saa 5:00 nyumbani kwake Masaki.
Mnaombwa kutuma waandishi wa habari na kwa wale wenye fursa kufika. Good morning.
Lakini baada ya waandishi kufika nyumbani kwake wakakutana na tangazo kuwa kuwa ameahirisha kuzungumza na waandishi hadi hapo itakapo tangazwa tena.
Kitendo hicho kimewakera sana waandishi wa habari.
Post a Comment