Imeendelea kuwa ishu ambayo kila mtu anaiongelea kwenye kona yake anachokiona sahihi, wapo wanaokosoa Mahakama kuamisha Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kupatiwa mtoto wake na Faiza Ally ambaye ni mzazi mwenzake.
Wa kwanza kuwasha kipaza sauti alikuwa Mbunge Martha Mlata >>> “Tuna Mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja Mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake”>>>
Ikaja time ya Mbunge David Kafulila >>> “Hii nchi ina mihimili mitatu, Bunge, Mahakama na Serikali… Tuheshimu maamuzi ya Mahakama”>>>
Waziri Saada Mkuya alikuwa wa mwisho kuongelea ishu hiyo hiyo >>> “Kama mama na mimi nilipoisikia ile taarifa nilipata uchungu, kila binadamu ana mapungufu yake lakini mtotto alelewe na mama yake”>>>
Post a Comment