
Dotto Mwaibale
Mwanamuziki wa miondoko ya Jazz kutoka nchini Italia Mwenye asili
ya Tanzania Chantal Saroldi anataraji kutumbuiza katika Hafla maalumu
ya kusherehekea Siku ya Taifa la Italia ambapo raia wa Italia waishio
nchini watajumuika pamoja kwenye viunga vya ubalozi wa Italia ili
kusherehekea Siku hiyo.
Mwanamuziki Chantal Saroldi mwenye asili ya Italia na Tanzania
alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro akitokea kabila la
Wachaga.
Chanty yupo nchini kwa ajili ya ziara maalumu ya Muziki ambapo
kesho anatarajia kutumbuiza katika hoteli ya Mediterraneo ya jijini Dar
esalaam na Juni 2 anataraji kutumbuiza katika hafla maalumu
inayoandaliwa na ubalozi wa Italia nchini ikiwa ni maadhimisho ya siku
ya Taifa hilo.
Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Scotto, alisema kuwa
katika kuzingatia kuwa mwanadada Chantal ni mwanamuziki mahiri waratibu
wa sherehe hizo wamemchaguliwa kuja kutumbuiza katika hafla hiyo kwa
kuwa ni nembo muhimu inayoziunganisha nchi mbili hizi za Tanzania na
Italia.
Katika hatua nyingine mwanadada huyo alisema kuwa anajilaumu kwa
kutojifunza lugha ya mama yake ambayo ni kiswahili, huku akibainisha
kuwa mikakati ni kujifunza lugha ya Kiswahili.
Mwanamuziki huyo amewahi kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya
dhahabu katika kipengele cha uhariri na uandishi wa nyimbo ikitolewa na
Disc Festival.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Post a Comment