Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri ndani ya Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita kwenye Shoo ya Instagram Party ambapo Wema alikuwa mmoja wa washiriki wa tamasha hilo lililohudhuriwa na mamia ya mashabiki hivyo walipata mshtuko waliposikia habari hizo njema kutoka kwa Madam.
Akiwa kwenye pati hiyo, Wema alipanda stejini kwa ajili ya kuongea na mashabiki wake na baadaye alipanda Luis ndipo Madam akaanza kummwagia sifa kedekede na kabla ya kumtambulisha rasmi kuwa ndiye ubavu wake.
Kwa kinywa chake bila kumung’unya maneno, Wema alidai kwamba Luis ndiye mwanaume ampendaye kwa sasa hasa akivua shati lake kwani ana vitu adimu ambavyo vinamfanya asimruhusu kuwa mbali naye.
LUIS NAYE
Baada ya sifa hizo, Luis naye alisema kuwa alipanda ndege kutoka Namibia hadi Dar kwa ajili ya kuja kujumuika na mwanamke ampendaye ambaye ni Wema.
Wema na Luis Manana wakifuatilia jambo. TEAM WEMA FULL SHANGWE
Utambulisho huo ulizua shangwe nyingi kutoka kwa mashabiki hasa Team Wema ambao kwa pamoja walionesha kusapoti uhusiano huo na hata baada ya kushuka walionekana kuwazonga huku wakipigana vikumbo kwa ajili ya kutaka kila mmoja kupiga nao picha. “Sisi Team Wema tumepitisha ile Team Haters (timu ya wenye chuki) wakale malimao kama alivyosema Gwajima (Askofu Josephat) kwamba kama kuna watu hawampendi Lowassa (Edward) basi wakale malimao,” alisikika mmoja wa Team Wema.
NI KWA MARA YA KWANZA BAADA YA DIAMOND
Usiku huo ulikuwa wa kwanza kwa mwaka huu kumuona Wema akimtambulisha mwanaume kwa mara ya kwanza kwenye tamasha kubwa kama hilo tangu alipoachana na Diamond ambaye kwa sasa anajivinjari na mwanamama Zarinah Hassani ‘Zari The Boss Lady’.Kuna madai kwamba baada ya wawili hao kuwa beneti tangu waliposhuka jukwaani walikwenda kulala hoteli moja kwa mujibu wa wafuatiliaji.
WALILALA WOTE HOTELINI
Chanzo chetu cha habari kilichokuwa ndani ya hoteli hiyo (jina linahifadhiwa) kilidai kwamba siku hiyo Wema na Luis waliingia hotelini hapo na kulala hadi kesho yake, jambo ambalo lilikuwa siyo kificho tena hasa kwa wahudumu na watu wote walioongozana na msafara wa wawili hao. “Kweli kabisa Luis anatoka kimapenzi na dada yetu Wema maana nimeshuhudia tangu jana, Wema alikuja hotelini na baadaye wakaondoka wote.
...Wakikumbatiana kimahaba. “Hata usiku wakati wanatoka Viwanja vya Posta pale Kitonyama walirudi na kulala pamoja, achilia mbali hiyo, Wema na Luis ni watu ambao wanaonekana kuwa katika mapenzi kwa muda sema tu Luis alikuwa hajapata nafasi ya kuja Dar,” kilisema chanzo hicho.
KUMBE LUIS ANAJUA KISWAHILI!
Baada ya kujiridhisha na uwepo wa uhusiano wa wawili hao, mwanahabari wetu alifuatilia kwa makini baadhi ya akaunti zinazotumiwa na Luis kwenye mitandao ya kijamii ambapo aligundua kuwa jamaa huyo amekuwa akimuweka Wema kwenye peji zake huku akimmwagia sifa na maneno ya kimahaba tena kwa Lugha ya Kiswahili.
Baadhi ya maneno aliyokuwa ameandika Luis katika peji yake ya Instagram akiambatanisha na picha zao yalisomeka: “Najaribu kumtuliza... Mtoto mzuri.“Huyu msichana anaweka tabasamu usoni mwangu.”
Post a Comment