Msuva ambaye amechukua tuzo mbili usiku wa leo, mbali na kuwa mchezaji bora Msuva amepewa tuzo ya mfungaji bora baada ya kutupia kambani jumla ya magoli 17 kwenye msimu uliomalizika Mei 9 mwaka huu na magoli hayo yaliisaidia Yanga kuibuka mabingwa wa ligi hiyo.
Lakikini kutokana na Msuva kuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, zawadi zake zilichukuliwa na wawakilishi wake ambaye ni baba yake mzee Msuva aliye ambana na mkewe mama yake Simon Msuva.
Msuva amewabwaga Mrisho Ngassa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye kinyang’anyiro hicho cha mchezaji bora wa ligi.
Nafasi nyingine ambazo zilikuwa zikiwaniwa ni pamoja na mlinda mlango bora ambapo tuzo hiyo imenyakuliwa na Shaban Kado (Coastal union) ambaye kwa sasa amesaini kuitumikia klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga akiwabwaga Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons) na Said Mohamed (Mtibwa Sugar).
Shabani Kado akipokea tuzo yake
Shabani Kado akipokea tuzo yake
Tuzo ya kocha bora imekwenda kwa Mbwana Makata aliyekinusuru kikosi cha Tanzania Prisons kisishuke daraja. Nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa na Goran Kopunovic (Simba SC) pamoja na Hans Van Der Pluijm (Young Africans).
Israel Mjuni Nkongo amenyakua tuzo ya mwamuzi bora akiwabwaga Jonesia Rukyaa na Samwel Mpenzu kwenye nafasi hiyo.
Mtibwa Sugar nao wamechukua tuzo ya timu yenye nidhamu iliyokuwa ikiwaniwa na Mgambo JKT pamoja na Wekundu wa Msimbazi Simba.
Wakati Huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake Jamal Malinzi, jana usiku lilitoa ofa kwa wazazi (baba na mama) wa Simon Msuva kuhudhuria mechi mbili za timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ itakapokuwa ikicheza dhidi ya Uganda kwenye michezo ya awali kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Afrika inayoshirikisha wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Malinzi ametoa ofa hiyo kwa wazazi wa Msuva ambaye jana alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya soka Tanzania bara iliyomalizika Mei 9 mwaka huu ikiwa kama zawadi na shukrani kwa wazazi hao mara baada ya wazazi wa Msuva kueleza njia ndefu aliyopita mtoto wao kufikia mafanikio anayoyapata hivisasa na wao kusimama nyuma yake kwa kila jambo gumu na rahisi alilopitia kijana wao.
Post a Comment