Kuna kitu watu wanashindwa kukikubali hapa. Alikiba anakabiliwa na pressure hii sababu ya kushindanishwa na Diamond. Mimi si muumini wa hizi team, lakini kama mchambuzi wa muziki na mtu ninayefuatilia sana muziki wa Tanzania, napenda watu watambue na kukubali kuwa Diamond na Alikiba hawako sawa tena. Mnamuonea tu Kiba kumfananisha na Diamond.
Katika maisha kutangulia sio kufika. Mwenzake yuko mbali mno na ili kuondoa pressure hii inayomkabili Kiba, ni kuacha kulazimisha kuwafananisha watu hawa wawili.
Maisha yatakuwa rahisi sana wakikubali ukweli huu. Wote ni wanamuziki wazuri na wote wana vipaji lakini bahati mbaya ni kuwa hawako level moja.
Just imagine mwenzie baada ya kutoa video ya ‘Nasema Nao’, ameachia video zingine mbili tena akiwa na wasanii wakubwa Afrika, Nana f/ Flavour na Nakupenda aliyofanya na Iyanya, lakini Kiba bado anadaiwa kavideo kamoja tu ka Chekecha! Ni kweli anaawangusha sana mashabiki wake lakini pengine huo ndio uwezo wake hivyo kwa kumtegemea afanye kama Diamond mnamuonea tu! Peace! (Mjumbe hauwawi)
COMMENTS ZA MASHABIKI HIZI HAPA:
sadickmwalongo7
Nimewambia watu mara nyingi diamondi anajua anacho kifanya anafaa kuigwa si mtu wa kujali sana maneno ya kukatish tamaa.kiba nae yuko vizur san tena san tu ila ni kweli kama alivyo sema wa mwanzo levo ya diamond ni nyingine ukilinganish umr wake so unagundua ni mtu tofaut sana ni mbunifu.kiba ulisem vumbi bila shak we ni vumbi sa2 au utafta tena maan hueleweki.unajaribu shindan na upepo wapo wa levo yako wengi si lazima diamondi mwisho wa siku unatafta aibu kaz zipi nyingi.huyu dogo achan nae tuanze upya tukague wapi tumekosea naamin tutashnda mzee mzima huo ndio ukweli.
moureenjo
Mi nadeclare interest napenda kiba anavyoimba pia ni shabiki wake sonce then ila alipoa muda mrefu sana toka ametoa wimbo na r kelly one eight, dai ni mjanja na anafanya juu chini asishuke hata kwa kutengeneza scandal kitu ambacho kiba hana hiyo
derique05
Penye ukweli huongo hujitenga.... well said aisee
queenmaggiexuan_one_n_only
ni kwel kiba kajisahau mno na kusema amkimbize chibu ni bdo sna
anethndosi
@udaku_special kunywa chochote kwabill yangu dah!!! Umeandika kitu chenye akili sana alaf mashabki ss ndowabaya tunajuwa kulingansha bla kuangalia unae mlinfansha nae yupo wap nampenda sana kiba napenda mzki wake saut yake ila aachane namambo yadai yatampa stress atashindwa kufanya ata icho kidogo alichonacho kwajili yamqshindano
Post a Comment