Habari kutoka nyumba ya jirani nchini Uganda ikufikie kwamba
aliyekuwa mume wa mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, tajiri Ivan Ssemwanga
anadaiwa kunasa penzi la shosti wa kufa na kuzikana wa mkewe huyo
aitwaye Stella Nankya,
Ijumaa Wikienda limetonywa.
Aliyekuwa mume wa Zari akiwa na mpenzi wake mpya ambaye ni shosti wa kufa na kuzikana wa Zari.
Ubuyu kutoka jijini Kampala nchini humo ulidadavua kwamba, Ivan na
Stella ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’, hivi
karibuni wamekuwa wakijiachia kimalovee kwa raha zao.
Zari akiwa na shosti wake Stella Nankya ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’.
Tukio la juzikati lililoacha gumzo ni pale wawili hao waliponaswa
wakiwa wamegandana kimahaba kwenye Ukumbi wa Ekitone uliopo Pretoria
nchini Afrika Kusini ambapo kulikuwa na tamasha la muziki.
Modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’ Stella Nankya akiwa katika pozi.
“Walikaa pamoja, walijiachia pamoja ziro ‘distansi’ kwani hakukuwa na
kitu cha kuwatenganisha kati yao. Kwa kweli walionekana ‘kapo’ ya
kupendeza mno,” alisema shuhuda wa tukio hilo na kukaririwa na gazeti
moja la nchini Uganda.
Kufuatia urafiki wa Stella na Zari walivyokuwa wameshibana, mashabiki
wao wamekuwa na maoni tofauti huku Stella akionekana msaliti kwa Zari.
Habari nyingine zilidai kwamba, Ivan ameamua kufanya hivyo ikiwa kama
kisasi au kumrusha roho Zari aliyezaa naye watoto watatu ambapo
anatarajia kumzalia Diamond siku chache zijazo.
Ilielezwa kuwa, Stella alipoulizwa kwa nini ameamua kumsaliti rafiki yake Zari kwa kutembea na Ivan alisema kwa kifupi:
“Sitaki kuwa karibu na mtu mkavu (Zari), na mimi nimeamua kuwa mkavu.”
Zari au mama kijacho na Stella walikuwa ni marafiki wakubwa ambapo
kuna wakati Zari alimpa sapoti ya nguvu Stella alipokwenda kuiwakilisha
Uganda kwenye mashindano ya urembo ya Miss Asia Pacific huko Seoul
nchini Korea Kusini ambapo walisafiri wote.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;
Filed Under:
Gossip
on Sunday, 17 May 2015
Post a Comment