Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Profesa Lipumba Amfananisha Lowassa na 'Kibaraka' wa CCM......Asema Uchaguzi wa Mwaka huu ni wa CCM 'A' ( Magufuli) Dhidi ya CCM 'B' ( Lowassa)


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kina wagombea wawili wanaowania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Madai hayo mapya ya Profesa Lipumba yametolewa siku tatu baada ya kujiuzulu uenyekiti CUF, akisema hiyo ni moja ya sababu za kuachia nafasi yake kutokana na uamuzi uliofikiwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu mgombea urais.

Akizungumza wakati akitangaza kujiuzulu wiki iliyopita, Profesa Lipumba alisema dhamira yake ilikuwa inamsuta kwa kuwaingiza ndani ya Ukawa watu kutoka CCM, waliokuwa wanapingana na maoni ya wananchi kuhusu rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba na kuwapa fursa ya kuwania urais.

Juzi usiku katika mahojiano aliyoyafanya na Azam TV kutoka mafichoni  alikojificha  ambako alisema anafanya utafiti, Profesa Lipumba alisema kumpa nafasi waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa kuwania urais kupitia Chadema ndani ya Ukawa, ni sawa na CCM kusimamisha wagombea wawili (Lowassa- CCM B) na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli- CCM A)

Katika mahojiano hayo ya simu, Profesa Lipumba ambaye wiki mbili zilizopita alimpokea Lowassa akisema ni mtu safi na kwamba, ufisadi ndani ya CCM ni mfumo  alisema katika kujiuzulu kwake hakutumiwa na CCM kuparaganyisha Ukawa, bali walikuwa tayari wameparaganyika.

“Ukweli ni kwamba tumejiparaganyisha wenyewe ndani ya Ukawa. Kwa hiyo Watanzania watakuwa na wanaCCM wawili wanaogombea urais wakati Ukawa tulikuwa na wagombea watatu... mimi, Dk Willibrod Slaa, (Katibu Mkuu wa Chadema) pamoja na Dk George Kahangwa (NCCR-Mageuzi) ambaye alikiri kuwapo makubaliano hayo.

“Tulikutana nyumbani kwangu tukakubaliana Dk Slaa apeperushe bendera ya Ukawa, lakini tumewekwa kando,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema yupo Rwanda kwa muda na anafanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa kiuchumi.

Pia alisisitiza kuwa hajahama nchi na kwamba wiki hii anatarajia kurejea nchini.

Agosti 6, mwaka huu Profesa Lipumba alijivua  uenyekiti wa CUF wakati mkakati wa vyama vya upinzani kushirikiana kushika dola ukiwa umeshika kasi.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 2025 24hours | Designed By Code Nirvana
Back To Top