Jumamosi ya wiki iliyopita, Chelsea ilitoka sare ya kufungana goli 2-2 dhidi ya Swansea City katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu England.
Wakiwa ndio mabingwa watetezi, Chelsea hawajasajili mpaka sasa zaidi ya Radamel Falcao ambaye yupo Stamford Bridge kwa mkopo.
Timu nyingine zimetumia pesa
kuboresha vikosi vyao, lakini Jose Mourinho amebaki na kikosi chake kile
kileambacho alikuwanacho msimu uliopita.
Msimu uliopita, Swansea walikufa mara mbili dhidi ya Chelsea, lakini msimu huu wameonekana kuwa na nguvu.
Je, hii ni dalili ya msimu huu kuwa mgumu kwa Mourinho?
Hivi unajua kwamba kikosi cha
Chelsea kilichocheza na Swansea msimu uliopita ndio kilekile
kilichocheza na tena na Swansea msimu huu kasoro mchezaji mmoja tu?
Angalia hapa utaona kikosi cha
Chelsea kilichocheza na Swansea Septemba 2014 na kilichocheza Agosti
2015, utaona kuwa kuna tofauti ya mchezaji mmoja tu.
Post a Comment