Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

CHADEMA YASAMBARATIKA LUDEWA: WANACHAMA WAKE ZAIDI YA 500 WAHAMIA ACT - WAZALENDO

 
Wanachama wa Chadema wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe wakiandamana kupinga maamuzi ya chama hicho kukata jina la mshindi wa kura za maoni na kumteua aliyeshindwa ,mbali ya kuandamana pia wanachama hao zaidi ya 500 walikihama chama hicho na kujiunga na ACT Wazalendo
Wanachama wa Chadema waliohamia ACT wazalendo wakiwa na mabango ya kukituhumu chama hicho kwa kukiuka Demokrasia
kadi na nyalaka za Chadema zikichomwa moto
Wanachadema wakiwa nje ya ofisi ya ACT Wazalendo ambako walifika kuomba kujiunga huko
kadi za chadema zikiteketezwa kwa moto
wana chadema wakiwa na mabango

Hasira za kukatwa kwa mshindi wa kura za maoni Ludewa
wanachadema wakijiandaa kwa maaandamano ya amani kujiengua na Chadema na kujiunga ACT wazalendo
Bango likimtaka aliyeteuliwa na chama kwenda kugombea jimbo la Hai kwa Mbowe
Mwanzo wa maandamano ya kujiengua na Chadema
wana Chadema katika maandamano ya kupinga uonevu ndani ya chama
Tuhuma dhidi ya Chadema Taifa
Wanachadema katika maandamano ya kupinga mshindi kutemwa
Wanachadema waliojiengua na kujiunga na ACT wazalendo wakiwa nje ya ofisi ya Chadema wilaya ya Ludewa
barua ya tuhuma za mteuliwa kutoa ahadi ya rushwa hii hapa
barua ikionyeshwa kwa wanahabari na wanachadema
Ni full jaziba kwa wana Chadema Ludewa
Wanachadema wakiwa nje ya ofisi ya chama wilaya walikokwenda kurudisha kadi kabla ya kuhamia ACT wazalendo
Aliyekuwa mwenyekiti wa BAWACHA wilaya ya Ludewa akionyesha kadi ya ACT wazalendo
Aliyeenguliwa Bw Haule akiwapongeza wana Chadema kwa kuhamia pamoja ACT wazalendo
Wanachadema wakirudisha kadi za chamna hicho na kujiunga na ACT wazalendo
Baadhi ya nguo na kadi zikiandaliwa kuchomwa moto
katibu wa ACT wazalendo Ludewa Alfred Ulaya akionyesha kadi za Chadema
Wanachadema wakijipata kuhamia ACT wazalendo
Kadi zikiwa zimekusanywa kwa kuchomwa moto
mwana Chadema akichoma moto kadi za Chadema Ludewa kupinga uonevu ndani ya chama hicho

Hivi ndivyo kadi zinavyoteketezwa kwa moto baada ya wana Chadema kujiengua na chama hicho na kujiunga na ACT wazalendo







Mabango ya kuagana na Chadema kwa wana Ludewa



Bango likionyesha Chadema kura za Chadema Urais X ,Ubunge X na udiwani X huku likimaliza kwa kusema msituchagulie


Mwanachama wa Chadema akiongea kwa jazba juu ya hali ya mambo ndani ya Chadema kabla ya kujiunga na ACT wazalendo

Ofisi ya Chadema wilaya ikiwa imefungwa wakati wanachadema walipofika kurudisha kadi zao

Kadi ya ACT baada ya kuhama Chadema
Makada wapya wa ACT kutoka Chadema

Aliyekuwa mshindi wa kura za maoni akionyesha barua nyenye siri nzito za mteuliwa kununua nafasi hiyo
Bw Haule akijiandaa kuchoma moto vifaa vyake vya Chadema kabla ya kujiunga na ACT wazalendo
........................................................................................................

*Wafanya Maandamano Makubwa. Wachoma Moto Kadi
* Ofisi ya Chadema Wilaya Nusuru Ichomwe Moto; Viongozi wakimbia; Watelekeza ofisi
Na MatukiodaimaBlog,Ludewa
WANACHAMA zaidi ya 500 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) Wilayani Ludewa Mkoani Njombe wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT Wazalendo wakipinga hatua ya uongozi wa juu wa chama hicho kukata jina la mshindi wa kwanza wa kura za maoni Bw. Ocol Haule na kumteua aliyekuwa mshindi wa pili katika mchakato huo Bw Bartholomeo Mkinga .


Wanachama hao ambao kutoka kata mbali mbali za wilaya ya Ludewa wamefanya maandamano hayo ya amani leo kuelekea ofisi ya Chadema wilaya huku wakitishia kuichoma moto ofisi hiyo baada ya viongozi wake kuifunga, kuitelekeza na kukimbia kunusuru maisha yao.


Wakizungumzia hatua hiyo ya kupinga maamuzi ya chama ngazi ya taifa wanachama hao Bi Hongera Gama, Taukile Mapunda na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) wilaya ya Ludewa Bi. Sophia Mtega walisema kuwa wanachama walikuwa na imani kubwa na mshindi wa kura za maoni kwani alifanya kazi kubwa ya kukijenga chama na sio huyo waliomuacha katika kura za maoni .


“Kinachoendelea sasa hivi ndani ya CHADEMA ni ufisadi mtupu,” alisema Bi. Gama akiongeza kuwa yeye binafsi alitoka CCM na kujiunga na Chadema kutokana na mapungufu yaliyokuwepo ndani ya CCM ila kinachoendelea kwa sasa ndani ya Chadema anajuta kuingia Chadema na hivyo ameamua kuhama chama hicho kumfuata mtu wao waliyemchagua popote atakakokwenda .


“ Mwenendo wa chadema kwa sasa ni wa ovyo zaidi kuliko chama chochote cha siasa hapa nchini tulikuwa tukishuhudia CCM watu wakikatwa ila leo ndani ya Chadema imekuwa ni kawaida kuona wale waliochaguliwa na wanachama kukatwa na watu wachache akiwemo mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Freeman Mbowe …..tumechoka tunahitaji kwenda kupata Demokrasia ya kweli ACT wazalendo sio ndani ya chadema”


Huku Bw Mapunda akidai kuwa siasa za ukabila zinaendelea kukitesa Chadema na kuwa suala hilo la ukabila na kuwakumbatia mafisadi ndilo ambalo linaendelea kukitafuna chama hicho pia siasa za ukanda na kukumbatia ufisadi imekuwa ni kawaida Chadema.


Hivyo alisema katika kuhakikisha wana Chadema wilaya ya Ludewa na kote nchini wanapinga siasa za ukanda na zile za kuwachukua watu wenye tuhuma za ufisadi kugombea ndani ya chama hicho ni lazima wanachadema kuungana kupinga hali hiyo kwa kuhama ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT wazalendo.


Aliyekuwa mwenyekiti wa BAWACHA wilaya ya Ludewa Bi Mtenga alisema kuwa uonevu na rushwa vimechangia wanachama na wananchi kukosa imani kabisa na chama hicho na sasa badala ya kuwa chama cha wanyonge kimekuwa ni chama cha wenye pesa na mafisadi jambo ambalo wao kama wananchi wa chini hawapo tayari tena kukaa ndani ya Chadema.


Akimkaribisha mgombea ubunge huyo aliyekatwa ndani ya Chadema Bw Haule na wanachama zaidi ya 500 wa chadema , katibu wa ACT wazalendo wilaya ya Ludewa Bw Alfred Ulaya alisema kuwa pia alipata kuwa kiongozi ndani ya Chadema wilaya ya Ludewa ila alihama pamoja na viongozi wengine kutokana na siasa za chuki ndani ya chama hicho na hatua ya kukumbatia ufisadi.


Hivyo alisema wanachama hao hawajachelewa kujiengua na chadema na kujiunga na chama cha ACT wazalendo kwani ni chama chenye misingi bora na chama pekee chenye malengo sahihi ya kulikomboa Taifa na Chadema na pamoja na umoja wao wa vyama vinavyo unda katiba ya wananchi (UKAWA) ni CCM B hivyo lazima watanzania wapenda mabadiliko lazima kuchagua ACT wazalendo.


Katibu huyo alisema kwa wanachama wote ambao wamejiengua na Chadema na kujiunga na ACT wazalendo wakiwemo makatibu na wenyeviti wa kata zaidi ya 10 waliojiunga na ACT wazalendo na viongozi wengine watakuwemo ndani ya chama hicho na vyeo vyao kama walivyotoka Chadema.


Kwa upande wake mgombea huyo aliyeenguliwa kugombea ubunge mbali ya kushinda kura za maoni Bw Haule alisema kuwa kimsingi aliyeteuliwa kugombea nafasi hiyo alikuwa amewaandikia barua baadhi ya viongozi ngazi ya wilaya ya kuwaahidi kuwapa pesa ,kufungua duka la vifaa mbali mbali pamoja na kuwahonga pikipiki barua ambayo aliinasa na kuwaonyesha wanachama hao.


Pia alisema kimsingi baada ya kuenguliwa kugombea nafasi hiyo alitaka kukaa kimya kama aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Dr Slaa ila akaona kukaa kimya bado si jibu na hivyo kuamua kujiunga na ACT wazalendo na kuweka uozo huo wazi.


Bw Haule alisema kuwa kwa sasa atahakikisha anazunguka jimbo nzima kufikisha kilio chake kwa wana Chadema na kupinga kwa nguvu zote wagombea wa udiwani na ubunge wa Chadema kupewa kura na kuwa kwa sasa uhai wa Chadema katika wilaya hiyo umekufa rasmi .
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top