Nadhani hata nyie mnalifahamu suala la kuoa au kuolewa ni mipango ya mtu mwenyewe pale mda wake utakapofika atafanya maamuzi yake mwenyewe hii ni kutokana na mtu kujipanga kwake.
Ni muda mrefu wazazi wananisumbua nioe na mimi bado sijampata mwanamke ninaemtaka,nikaona ili niwaridhishe wazazi nikaona ngoja niwapake mafuta kwa mgongo wa chupa.
Nikachukua maamuzi nikaenda sehemu zile wanazojiuza wadada wale wa High quality nikamchagua mmoja mzuri sana nikamueleza nia na dhumuni langu tukakubaliana nimlipe kwa dau flani niende nae kama mpenzi wangu na awe na nidhamu zote kwa wazee.
Basi nilifanikiwa na walifurahi sana tafrija fupi ikapita Mara wanandugu wakaitwa njooni mmuone mchumba wa flani kila mmoja alimpenda huku nikiambiwa umechagua kifaa.
Niliona kama maigizo flani ambayo mbeleni pataishia pabaya na kweli ikawa hivyo.Sasa nimeletewa taarifa kwamba ndugu wamekaa kikao wameshapanga kila kitu kuhusu suala la harusi hadi tarehe.Nimechanganyikiwa vya kutosha na yule kahaba kachapa zake kona
Nipeni mawazo jamani nifanye nini?
Post a Comment