Afisa habari wa Simba Hajji Manara amesema Azam walipanga jambo hilo kwasababu Singano alishasema kwenye kikao cha kwanza kuwa Azam ni miongoni mwa klabu ambazo zilikuwa zikimuhitaji wakati bado akiwa na mkataba na Simba.
“Hili jambo limepangwa, na mkiuliza nani amelipanga mnamajawabu. Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji juzi imemtangaza Messi ni mchezaji huru wamevunja mkataba wetu, leo amesaini Azam. TFF hawajatuletea barua, huyu mchezaji mpaka juzi sisi tunatambua ni mchezaji wa Simba mpaka hivi sasa barua ‘official’ haijaja ndio maana nasema hili jambo lilipangwa sikunyingi na TFF wanalijua hili”, amesema Manara.
“Itawezekana vipi mchezaji ambaye sisi barua hatujapata ya kuvunjwa kwa mkataba wake asaini kwenye klabu nyingine? Kwakutopewa barua mpaka leo maana yake nini? Sisi tunashindwa kutoa ‘official statement’ ya klabu na tunashindwa kuchukua hatua zozote wakati hawajatuletea barua tayari mchezaji kaenda Azam”, Manara alihoji
“Na kwenye kikao aliwataja Azam kuwa ni miongoni mwa klabu ambazo zilikuwa zinamsumbua”, alimaliza.
Leo mchana Singano amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu ya Azam FC baada ya mkataba wake na Simba kuvunjwa na kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji kufuatia Simba kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya mkataba kati ya mchezaji na klabu.
Post a Comment