Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani
Papa Francis amewatawaza watawa wawili wa Kipalestina walioishi katika
karne ya 19 wakati wa utawala wa Ottoman kuwa watakatifu.
Watawa
hao wawili walioishi miongoni mwa jamii ya wapalestina waarabu ,bi Marie
Alphonsine Ghattas na Mariam Bawardy watakuwa miongoni mwa watakatifu
watakao tawazwa hii leo katika ukumbi wa kanisa kubwa la papa Francis la
St Peter's Square iliyoko Rome.Hatua hii inatazamwa na wengi kama chambo cha kuwavutia wakristu katika maeneo ya mashariki ya kati ambapo wakristu wanahujumiwa na jamii.
Hapo jana Papa Francis alifanya mazungumzo na rais wa wapalestina Mahmoud Abbas katika makao makuu ya Vatican.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alimtunuku Abbas medali ya Amani huku akimtaja kuwa ''malaika wa amani''
Watawa hao Marie Alphonsine Ghattas - aliyezaliwa katika familia ya kipalestina mjini Jerusalem alianzisha huduma ya watawa ya - Rosary Sisters, ambayo hadi wa leo inaendesha shule za chekechea na zile za msingi.
Bi Mariam anasemekana kuwa alitenda miujiza miongoni mwa jamii yake huku akitambuliwa kwa kuonekana na alama za ishara ya kusulubishwa kwa Yesu Kristo msalabani.
Wawili hao waliishi katika enzi ya Ottoman ambapo wanawake hawakuwa na semi katika hali halisi ya maisha lakini waliibuka kuwa mifano ya kuigwa licha ya kuishi maisha ya uchochole na magonjwa mengi.
Kutawazwa kwao kunatarajiwa kuweka msingi yao kutambuliwa kama watakatifu kutoka kwenye chimbuko la ukristu.
takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wakristo imedidimia kwa asili mia 2% katika eneo la Palestina na Israili.
Hii inatokana na umaarufu mkubwa wa Waislamu na Wayahudi ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wapigana na kuwalazimu wakristu kutorokea mataifa salama kuepuka vita.
Post a Comment