Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Sentensi Nyingine 22 za Faiza Ally Kuhusu Mavazi yake, Mtoto, Dini, Umaarufu.. Anajuta? (Audio & Pichaz)

Kama uko karibu na stori za TZ najua hautakuwa umesahau kuhusu ishu ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mzazi mwenzake, Faiza Ally.. Mbunge huyo hakuridhishwa na mavazi ambayo mzazi mwenzake alionekana nayo sehemu mbalimbali akaipeleka ishu Mahakamani kwamba kutokana na mama wa mtoto anavyoonekana yeye haridhishwi mtoto kuendelea kulelewa na Faiza.
IMG_2363
Chanzo cha yote ilikuwa ni aina ya mavazi, leo kwenye show ya #Nirvana @EATV Faizaalikuwa kwenye Interview na ishu kubwa ilikuwa kuhusu mavazi yake >>>>“Napenda kuvaa vitu ninavyovaa, sina mavazi special naweza kuvaa vyovyote, niliipenda idea ya kuvaa nepi (diapers) na sina tatizo nayo kabisa
IMG_2356
Faiza ni mama wa mtoto mmoja wa kike, kwenye upande wa malezi ikoje? >>> “Mimi ni mama mzuri sana, ninamtazama mtoto wangu saa 24… mavazi yangu hayaingiliani kabisa na malezi ya mtoto wangu… namlea kwa mazingira ya heshima, heshima na nguo ni vitu tofauti… ninavaa mavazi ninayopenda na bado nina heshima kwa watu. Sio lazima kila mtu akubali ninachofanya, ninapofanya kitu kwa watu kukubali au kukataa ni matatizo yao” >>> Faiza Ally.
IMG_2354
Kuna kitu chochote anachojutia kutokana na mavazi yake? >>> “Sina ninachojuta, niko sawa… tukio ambalo sijafurahia ni moja la kupelekwa Mahakamani na kunyang’anywa mtoto wangu kitu ambacho ninakifanyia kazi  na kinaenda vizuri.. sioni tukio  baya zaidi ya watu kunitukana na ni kawaida… ninaenjoy na ninapenda mavazi yangu” >>>>
IMG_2366
Haya ndio maneno yake kuhusu nguo aliyoivaa kwenye KTMA 2015 >>> “Idea ilikuwa ni nzuri mpaka pale ambapo nguo iliachana… lengo lilikuwa sio kuacha makalio wazi, ile nguo baada ya kukaa kwenye gari ilishuka na sehemu ya makalio ikabaki wazi… Wakati natoka nyumbani ilikuwa imekaa tu vizuri, nilivyoshuka kwenye gari sikujiangalia, nilipofika red carpet nikapigwa picha” >>>>
IMG_2351
Anatoka kwenye familia inayofuata Dini? >>> “Baba yangu sijawahi kumwona anakwenda Msikitini, sio kwamba naikana dini lakini sijazaliwa kwenye familia ya kidini.. maisha yangu yako hivi miaka yote na hakuna kilichobadilika kwenye maisha yangu… nafurahia maisha yangu” >>>>
Huu ndio ushauri wake kwa wasichana kuhusu ishu ya fashion za mavazi >>>> “Wasichana wajue kwamba kilicholeta gumzo ilikuwa bahati mbaya, ila wawe huru wavae vitu wanavyovifurahia ila isitokee kama ile… kuna mavazi navaa na kuna mavazi siwezi kuvaa” >>>>
IMG_2352
Matukio ya mavazi yake yamempa umaarufu? Amepanga kufanya chochote? >>>> “Sijapanga chochote, sikujua kama itakuwa ni umaarufu… mimi ni mwigizaji na ninaandika kitabu, labda kwa kazi zangu hizo… kipande kilichoonekana sio maisha yangu yote, ni sehemu ya mwili… Faiza ni mwanamke mzuri, anayejielewa, mwenye akili timamu, mama bora, anayejipenda, mtu wa watu” >>>>  Faiza Ally.
IMG_2367
Kwenye Interview hiyo alikuwepo pia mwanamitindo Ally Rehmtullah, haya  ndio maneno yake kuhusu nguo ya Faiza >>>> “Ubunifu wake ulikuwa mzuri labda mawasiliano kati ya yeye na mbunifu wake hayakuwa mazuri, vazi kama lile kwa utamaduni wetu lazima watu watashtuka watakusema, ni muhimu kujua yeye mwenyewe Faiza alikuwa anataka nini… Naamini ilikuwa bahati mbaya, ingekuwa ni mimi ile gauni nisingevaa” >>>> Ally Rehmtullah.
Majibu ya Faiza Ally yako pia kwenye hii sauti niliyorekodi kipande cha Nirvana mtu wangu, unaweza kuplay kumsikiliza mwenyewe
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top