Mpango
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumtangaza kada wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa, kujiunga na chama hicho
uliotarajiwa kutekelezwa jana, umekwama huku kukiwa na taarifa za
mgawanyiko ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wiki
iliyopita, Mtandao huu uliandika taarifa kwamba Chadema walipanga
kumtangaza Lowassa Jumapili ya jana baada ya kumaliza mazungumzo naye,
lakini hilo lilishindikana.
Taarifa
kutoka ndani ya Chadema zinadai kuwa huenda kada huyo ambaye
mustakabali wake ndani ya CCM uliingia dosari baada ya jina lake
kuondolewa alipokuwa akisaka urais, sasa huenda akatangazwa rasmi wakati
wowote wiki hii.
“Kwamba
anakuja Chadema hiyo si siri tena, lakini ule mpango wa kumtangaza leo
(jana) haukufanikiwa kutokana na kuwapo kwa vikao tofauti muhimu vya
vyama viwili ndani ya Ukawa, Chadema na CUF,” alisema mtoa habari wetu ndani ya Chadema.
Jana,
Chadema waliitisha mkutano wa dharura wa Kamati Kuu jijini Dar es
Salaam wakati ambapo CUF nao walikuwa na mkutano wa Baraza Kuu huko
Zanzibar, wote wakijadiliana suala moja tu; urais ndani ya Ukawa.
Vikao
hivyo vilivyogubikwa na usiri mkubwa vilitarajiwa kumalizika jana
mchana na kisha jioni wenyeviti wenza wa Ukawa walipanga kuzungumza na
wahariri wa vyombo vya habari, lakini mkutano huo uliahirishwa kutokana
na kushindwa kumalizika kwa wakati vikao hivyo nyeti.
Akizungumza
na mtandao huu jana, Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya,
alisema kwa ufupi kuwa kilichokuwa kikijadiliwa na chama hicho kitawekwa
hadharani leo, huku Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa
Mohamed naye akisema: “Tutawafahamisha kinachozungumzwa baada ya kikao kumalizika.”
Watu
wa karibu na CUF wanadai kuwa uongozi wa juu wa chama hicho, hasa
Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba, hadi jana hakuwa akiafiki ujio wa
Lowassa Ukawa.
“Sijui
itakuwaje lakini kama msimamo wa Profesa ukiendelea hivi, sioni namna
gani CUF itaendelea kuwamo ndani ya Ukawa. Kwanza kura ambazo huwa
anazipata kwenye urais nazo ni muhimu sana kwani husaidia chama kupata
ruzuku.
“Sasa
iwapo hatagombea na labda akagombea Lowassa kupitia Chadema ndani ya
Ukawa, basi suala la ruzuku litaleta balaa kwani ndizo fedha
zinazosaidia kuendesha ofisi za CUF Tanzania Bara,” alisema
mwanachama mmoja wa CUF, akizungumzia utata uliokigubika chama hicho
unaohatarisha maisha ya Ukawa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka
huu.
Kwa
upande wa Chadema, mtandao huu ulihakikishiwa jana kuwa wao hawana
shaka na ujio wa Lowassa, wakiandaa mazingira ya kumsafisha mbele ya
wananchi kwa madai kuwa kilichofanya aonekane mchafu ni mfumo ndani ya
CCM na wala si yeye kama Lowassa.
Ingawa
kumekuwapo madai kuwa wanafamilia ya Lowassa na marafiki zake wachache
wamekuwa wakimshauri kutohama CCM, lakini Lowassa ndiye mwenye uamuzi wa
mwisho na kwamba mmoja wa rafiki zake wakubwa na mfanyabiashara maarufu
nchini amewahi kusikika akikiri kuwa ameshindwa kumshawishi rafiki yake
huyo kubaki CCM.
Source; Mpekuzi blog
Post a Comment