KAMBI
ya aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), imeanza
kusambaratika baada ya wafuasi wake kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo.
Wafuasi
wake hao wakiongozwa na diwani aliyemaliza muda wake katika Kata ya
Kunduchi, Janeth Rithe, wamejiunga jana ACT-Wazalendo na kukabidhiwa
kadi na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa.
Wengine
waliopewa kadi za ACT ni Mary Mongi aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji Bawacha, Jimbo la Kawe, James Wambura (Katibu wa mbunge Kawe)
na Manase Busa aliyefanikisha kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Mdee
anaingia bungeni katika uchaguzi wa 2010.
Wamo
pia Katibu Bawacha Tawi la Wazo, Modesta Kalukula na Sizya Issa, Yamoyo
Salehe, Sheilah Khamis, Tabia Mohamed, Ashura Salehe, Sophia Makoba na
Fatuma Mikidadi.
Mbali na hao, chama hicho pia kimepokea wanachama wengine 198 kutoka CCM, Chadema na NCCR-Mageuzi waliojiunga kutoka jimbo hilo.
Akizungumza
baada ya kuwapokea, Msafiri alisema wanachama hao wameungana ili
kuendeleza uzalendo kwa Taifa, hivyo chama hicho kinawakaribisha na
wengine.
Post a Comment