Rapper Afande Sele amesema wasanii hawajanufaika na ubunge wa Joseph
Mbilinyi aka Sugu licha ya kumsaidia kumpigia kampeni katika uchaguzi
uliopita.
Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio, Afande alisema Sugu
ameshindwa kuwatumikia wasanii na kujinufaisha yeye mwenyewe.
“Sisi tuliamini akienda kule ndio mdomo wetu, kasahau kabisa wasanii
wenzake,” alisema.
“Kipindi ambacho wasanii wa antivirus wanalalamika
kwamba kawatosa porini, akasema yeye sio mbunge wa wasanii ni mbunge wa
Mbeya. Huyu ni msaliti kwa wenzake, sasa mtu msaliti namna hii jinsi
kumuondoa ni sisi kuamua kuingia bungeni wenyewe kupigania maslahi
yetu,” aliongeza.
Baada ya kauli hiyo, Sugu amemjibu kwa kusema kuwa yeye hakuwa mbunge
wa wasanii bali alikuwa mbunge kwaajili ya watu wake wa Mbeya mjini.
“Nafikiri hafuatilii bunge, unajua uzuri wa vitu vya bunge vinaenda
kwa rekodi, labda atakuwa hafuatili bunge. Lakini kwa wanaofuatilia
bunge wanajua. Mimi sio mbunge wa wasanii, mimi ni mbunge wa Mbeya
mjini,” alisema Sugu.
“Kwahiyo chochote ninachokifanya bungeni ninakifanya kwa mapenzi
yangu na pia kama waziri kivuli. Kwa msanii anayefanya kazi sawa ila kwa
mtu anayelala lala kama yeye lazima atakufa njaa. Lazima utakufa njaa
lakini kwa msanii kama Professor Jay, msanii kama Shetta wana-
appreciate kazi ambayo tunaifanya bungeni kwa kauli zao.”
Post a Comment