Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MAKAVU LIVE: KAMA HUMPENDI, KWANINI UZAE NAYE?!

HABARI zenu wapendwa wasomaji wa safu yetu hii, tunaokutana kila wiki katika kuburudishana, kuelimishana na mara nyingine hata kufundishana. Najua wapo baadhi ya wasomaji hawakosi kabisa sehemu hii kwa sababu yanayozungumziwa, ama yamewakuta, au wanashiriki hadi sasa, au yaliwahi kuwapata watu wao wa karibu.
Katika jamii tunayoishi kuna mambo mengi yanayoendelea ambayo huonyesha jinsi gani wawili walivyohusiana kimapenzi, lakini hujitokeza baada ya mapenzi yao kuharibika. Utamaduni au mazoea ya uhusiano wa kimapenzi kwa jamii yetu yanaonyesha kuwa wawili wanapotofautiana, huanza kutoleana maneno yasiyostahili.
Watu kuzaa bila ndoa siku hizi linaonekana kuwa ni jambo la kawaida na hii inatokana na mfumo wetu wa maisha, kwani wapo ambao walijaribu maisha ya ndoa, lakini mambo yakawa magumu kutokana na vipigo, manyanyaso na mateso mengine mengi.Cha ajabu asilimia kubwa ya wazazi hawa, wamekuwa wakitoa kauli kwamba hawawapendi wenza wao japokuwa walizaa, kauli ambazo naamini siyo sawa.
Utakuta mwanamke akisema; “Ohoo! Simpendi yule mwanaume kama nini, basi tu ilitokea nikazaa naye.” Sidhani kama maneno haya yana mbolea kwa sababu ni jambo la kawaida mtu kuridhika urafiki unapovunjika kwa sababu ni jambo la kawaida. Hata wanawake hawatakiwi kueleza kwa staili hiyo kwa sababu wakati wakiwa kwenye uhusiano, kila kitu kilikwenda sawa.
Suala la kuzaa hakuna bahati mbaya, watu huwa wanajifariji tu lakini cha msingi ni kwamba mpaka unaamua kuzaa na mtu tambua kwamba ulimpenda na umekubaliana na hali yoyote itakayojitokeza katika maisha ya kumlea mtoto wenu.
Ninavyojua, kama mtu anashiriki mapenzi na mtu asiyempenda, huchukua tahadhari nyingi ili kuhakikisha suala la ujauzito halitokei. Maana wengine hujikuta wakishiriki na mtu kwa sababu tu ya shida ya wakati huo, kama vile ugumu wa maisha, shinikizo la kazi, kesi au vingine.

Kama unashiriki na mtu kwa staili hii, zipo njia za kujihami kuhakikisha ujauzito hautokei, kama vile kutumia kinga na mara nyingi mapenzi ya namna hii huwa ya muda mfupi, labda kama ni kubakwa.Kwa maana hiyo, suala la kuzaa na mtu usiyempenda halipo. Kutoa maneno hayo ni kama kuwapa mkosi watoto au mtoto mliyezaa ambaye anatambua kuwa wazazi wake ni watu waliopendana.

Kitu cha msingi ni kwa wapenzi ni kutambua kuwa katika mapenzi, kutengana ni jambo la kawaida kabisa katika jamii zote duniani. Hakuna ajabu yoyote kwa jambo hili na kwa sababu hiyo, ni jambo la kushangaza kumkuta mmoja wa wapenzi waliopendana hadi kuzaa, eti leo akilalamika kuwa hakumpenda mwenzake!
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top