Malkia anayemiliki Kampuni ya Endless Fame
Production, Wema Isaac Sepetu na Mshindi wa Big Brother Africa 2014/15,
Idris Sultan ambao wamekuwa marafiki wakubwa katika siku za hivi
karibuni, nusu wazichape kavukavu baada ya kupishana kauli huku wivu wa
kimapenzi ukitajwa.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita nje ya Hoteli ya
Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar
ambapo kwa pamoja walikuwa wamehudhuria sherehe ya utoaji Tuzo za Watu.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tafrani ya wawili hao kutaka kukunjana
ilitokea baada ya kumalizika kwa shuguli hiyo ambapo Idris alimpora Wema
tuzo yake aliyoshinda na kwenda nayo kwenye gari lake.
Ugomvi huo ulipamba moto na kusababisha watu waliokuwa wakiwashuhudia
kutaharuki ambapo Wema alikwenda kwenye gari lake lililokuwa
likiendeshwa na Petit Man lakini Idris alimfuata akionekana kumuonea
wivu na kumtaka apande gari lake waondoka jambo ambalo Wema alilitolea
nje na kumfungia kioo.
Baada ya kuona Wema amemtolea nje, Idris alikwenda kwenye gari lake
na kuliegesha mbele ya gari la Wema ‘kum-block’ ili asiondoke ambapo
alishuka na kumwambia Petit Man ahakikishe anamfuata kwa nyuma jambo
ambalo Petit Man alishindwa kulitekeleza baada ya Wema kukataa.
Baada ya kushuhudia vurugu hizo, mwanahabari wetu alimfuata Wema ili
kujua kilichotokea ambapo mwanadada huyo alisema kuwa haelewi ni kitu
gani ambacho kilimkuta Idris siku hiyo maana kama angekuwa anakunywa
pombe, angesema labda alizidiwa lakini kwa kilichotokea hadi leo hajui
ni kipi kilimkuta.
“Yaani hata sielewi Idris alifikwa na nini maana amefanya mambo ya
ajabu sana na mara ya kwanza nilijua utani lakini nilimshangaa zaidi
baada ya kukomaa hadi kufikia hatua ya kuni-block na gari lake huku
akitaka niondoke naye wakati kila mtu alikwenda pale kimpango wake.
“Mimi
nadhani kuna utoto fulani bado anao na unamsumbua,” alisema Wema lakini
Idris hakupatikana kusema chochote.
Credit: Gpl
Post a Comment