KWANINI USINDIKIZE WENZIO!! ni sawa na kwako kuwe ILALA halafu kwa kukwepa mashimo ukaona upite MBEZI BEACH ambapo uliskia njia ni nzuri kwa kutegemea ufike ILALA, IMPOSSIBLE! Kitakachotokea MBEZI utakaa kwa muda mfupi tu kusubiria MUDA uanze tena safari ya kupatafuta/kurudi ILALA!! WASTAGE OF TIME! This is the BIG reason in my life SIJAWAHI KUSHINDANA NA SISHINDANI, ila NAFANYA..Nafanya kile nachotakiwa kufanya.. bila PRESSURE wala wasiwasi sababu naamini safari ya kwangu ni YANGU!! Ina njia zangu na mwisho wangu..
Kwa wanaonijua huwaga SINA STRESS NA VITU!! kushindana ni kupoteza mwelekeo wa ya kwangu.. siangalii nani anafanya nini ili nifanye but naangalia natakiwa kufanya nini kwa muda husika,Sioni vibaya kwa mafanikio ya yeyote yule, Naamini nna ya kwangu..SIIGIZI maisha wala kuweka TASWIRA ama ATTITUDE nisiyokuwa nayo..I am who I am!! Nataka mtu anitambue kwa cha kwangu.. kunichukia ama kunipenda iwe kutokana na tabia yangu ya ukweli na sio ile plastic ya kujivisha.. Na kama kuna chochote nnachotakiwa kukipata basi nikipate kwa NILIVYO na sio kwa sira nisiyokuwa nayo ambapo baadae itakapogundulika tofauti ikawa tofauti!! KIKUBWA Dont stress over someone else's life..
RELAX!! sababu hata siku moja Huwezi kubadili ukweli wa KWAKO!! KWAKO HAPABADILIKI.. na hata ushinde na kulala nyumba za jirani lakini mwisho wa siku lazima urudi KWAKO..TENGENEZA KWAKO!! Hakuna mwisho mbaya.. Ila tunautengeneza tunapopita njia tofauti na tunazotakiwa kupita ili tufike, NJIA ZA WENZETU.. Lazima utokee pasipokuhusu ambapo automatic hapatakuwa pazuri KWAKO ila kwa PANAEMUHUSU.. NATAKA NIFIKE KWANGU.
Zamaradi mtetema ambaye ni mtangazaji na muaandaaji wa filamu za kibongo aliandika hayo kwenye ukurasa wake mtandaoni na kungwamkono na watu wengi.
Post a Comment