Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Afungwa Miaka 130 jela kwa kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 ukimwi

Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 130 jela kwa kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 ukimwi.
Katika kikao hicho Mahakama kuu ya Kenya mjini Kisumu imempata na hatia bwana John Okewo mwenye umri wa miaka 25 na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye jina lake limebanwa. Hakimu mwandamizi Aswani Opande alimpata na hatia bwana Okewo kwa kumabaka mtoto huyo na akamhukumu kifungo cha miaka 100 jela.

Katika shtaka la pili hakimu huyo mkuu wa eneo la Tamu lililoko Muhoroni alimhukumu mstakiwa kifungo cha miaka mingine 30 kwa kumuambukiza msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 ugonjwa wa Ukimwi. Hakimu alimpata na hatia bwana Okewo kutokana na kukiri makosa yake mwenyewe.

Upande wa mashtaka unasema kuwa bwana Okewo alimpa mtoto huyo pipi na biskuti mnamo tarehe 27 mwezi Machi kabla ya kumdanganya hadi akaingia chumbani mwake. Yamkini Okewo aliwaambia wachunguzi kuwa alimdhulumu mtoto huyo mara kadha.

Mtoto huyo alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi na ''kumlalia'' Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 anaendelea na matibabu maalum ya wanawake baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo. Alipopewa fursa ajitetee, mshtakiwa aliomba asamehewe kwani ni ''shetani aliyemdanganya'' kutenda maovu hayo.

Hata hivyo Hakimu akakataa kabisa kumuonea huruma na akamhukumu kifungo cha miaka 130 jela ili iwe funzo kwake na kwa wengine wenye mawazo potofu kama yake. Alipewa siku 14 kukata rufaa.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top