Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Nimemtoa Out Kaja na Marafiki zake Watatu...Kilichofuta Baada ya Hapo ilinibidi ni Escape From Sobibo

Jana jioni nilipotoka kazini nilipitia recreation place moja hivi nipate moja moto moja baridi wakati nikisubiri foleni iishe Ingawa sina Gari ila kwa kawaida ikifika saa mbili usiku kidogo fujo za dala dala posta -makumbusho zinakua zimepungua..

Basi nikiwa hapo recreation nikampigia simu mrembo mmoja hivi staff mwenzangu kazini ambae nimekua nikimfuatilia sasa kwa wiki kadhaa nikamwomba apite nilipo tupate japo bia mbili Mbili huku tukizungumza

Cha kushangaza kaja na mashoga zake watatu na yeye Wa nne baada ya kuona nimeshtuka akajibalaguza kwa kusema eti amekutana nao hapo nje tu
Wakaagiza Windhoek lager mmoja akaagiza savana dry
Nikasema moyoni kwa kijita lelo ni lelo
Walipofika bia ya tatu kila mmoja huku wakiongea stori zao za kina diamond na Ali kiba zisizo na kichwa wala miguu wawili wakainuka kwenda jikoni kutazama nyama choma nilisikia kama ganzi miguuni na ndipo hapo nilipoanza kufikiria escape from sobibo

Wakati nimeanza kupanga escape plan warembo hao walikua bia ya sita kila mmoja wadada wananyonya bia sijawahi ona, mm nipo bia ya tatu tena safari nikinywa kwa kuichungulia
Yote tisa, kumi wakaagiza kongoro la kukatia pombe wakati wakisubiri nyama choma iive ambayo sikutaka hata kujua ni kiasi gani

Ilikua ni Saa mbili na nusu usiku nilipojifanya nakwenda kuongea na simu nje nilipofika nje ya bar hiyo iliyokaribu na billicanas club nilipiga hatua ndefu kuelekea posta Mpya huku nikitazama nyuma kwa hofu kama kuna mtu ananifuata, nikatokea nmb phonex house na mungu si Athuman hili hapa dala dala la makumbusho posta likiwa na abiria wachache nikadandia hill hilo na kupiga ishara ya msalaba kwa kufanikiwa kutoroka salama
Nikazima simu hadi saa sita usiku ndo nikaiwasha na kukutana sms kama 30 hivi za matusi kutoka kwa yule binti Wa kazini, akiniita majina yote mabaya kuanzia firauni na mengine mengi
Kwamba wakiitwa wanaume nawe utatoka?
Kwamba janaume suruali tu
Kwamba Aliniona Wa maana kymbe sina lolote

Leo asubuhi amenikuta nimeshakaa kwa meza yangu amefika akasimama mbele yangu akaniangalia kwa macho makali sana na akavuta msonyo mrefu sana na kwenda kwenye idara yake
Nahisi ndo ntakua nimekataliwa hivyo

Wakuu msichana anakuja kunikomoa hivyo huku anaujua kabisa mshahara wangu tupo ofisi moja anajua mm ni karani tu Wa kawaida
Wote mm na yy net yetu inalingana
Mabinti mjirekebishe sio vizuri kwa kweli
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top