Kumbe! Machoni pa wengi maswali yaliibuka miongoni mwa mashabiki wa
mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan
‘The Boss Lady’ baada ya kumuona akiwa ‘klozi’ na Bosi wa Bongo Stars
Search (BSS), Rita Paulsen ‘Madam’ kwenye shoo ya Zari All White Party
iliyofanyika juzikati kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
Madam Rita akiwa katika pozi na Zari walipokua kwenye Zari All White Party.
Katika ‘iventi’ hiyo, Madam Rita alikuwa beneti na Zari hivyo baadhi
ya watu walikwenda mbali zaidi na kudhani labda Madam alikuwa kama
bodigadi’ wa Zari ili kusaidia linapokuja suala la kumwaga ung’eng’e
a.k.a kutema yai lakini
Ijumaa Wikienda limefanya kazi yake na kubaini kwamba wawili hao ni ndugu kabisa.
Wakiwa katika pozi.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba Zari na Madam Rita si ndugu
wa tumbo moja ila mama zao ndiyo wenye undugu wa damu kwani wanaitana
binamu.
Ilifahamika kwamba, Zari amekuwa akikutana na Madam Rita mara kwa
mara anapokuwa Bongo, ikiwa ni pamoja na kushauriana mambo kibao ya
kimaendeleo hasa katika suala zima la kuona fursa kwenye ishu za
burudani.
Madam Rita, Diamond na Zari wakiwa katika picha ya pamoja.
Imebainika kuwa ukiachana na kukutana Bongo, ndugu hao wamekuwa wakikutana Sauzi kwenye mishemishe zao za kusaka ‘mahela’.
Kwa mujibu wa Madam Rita, mbali na undugu, anamkubali Zari katika
pilikapilika za kusaka maisha lakini pia Zari naye anamkubali Madam Rita
kwa harakati zake za utafutaji na kupambana na umaskini.
“Zari ni mwanamke mtafutaji na ni ndugu yangu kabisa. Unajua pale
Mlimani City watu walikuwa wanauliza tupoje, wengine walidhani nipo na
AKA (msanii wa Afrika Kusini) lakini ukweli ni kwamba mimi na Zari
tunafahamiana vizuri,” alisema Madam Rita.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;
Filed Under:
Gossip
on Monday, 11 May 2015
Post a Comment