
Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven
Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka kuwa ili azae,
staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatakiwa alale juu ya
kaburi.
Hayo yanakuja siku chache baada ya Wema aliyewahi kuwa mchumba wa
Kanumba kudai kusumbuliwa na tatizo la kukosa uwezo wa kuzaa hivyo mzee
huyo kujiongeza na kusema ni kwa sababu alitoa mimba ya mwanaye huyo.
Akizungumza na waandishi wetu, baba huyo alisema kama kweli Wema
alitoa mimba ya Kanumba basi atakuwa alijilaani kwa sababu ukoo wao
ukitoa mimba unaweza kufa au kujilaani (kutokupata mtoto) hivyo
anatakiwa kutambika kwa kulala juu ya kaburi la mama mkubwa wa Kanumba
ambaye ni bibi wa babu wa mzee Kanumba.
Alisema sambamba na hilo, Wema atatakiwa kurithiwa na ndugu wa Kanumba (kati ya kaka au mdogo wake).
“Kwenye ukoo wetu ukitoa mimba kuna mambo mawili, moja ni kufariki
dunia au ‘kujikila’ (kujilaani) kwa kutokuzaa, pengine ndicho
kilichomtokea Wema,’’ alisema baba Kanumba.
Mzee huyo alisema kuwa mama mkubwa huyo
alishafariki dunia kwa hiyo yeye na marehemu Kanumba walipaswa kwenda
kaburini kwake kufanya tambiko zito, wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya
kiasili na mikononi wameshika vibuyu, jambo ambalo lingempasa Wema
kukaza moyo.
Alisema kuwa wakiwa kaburini hapo, Wema alitakiwa achotewe
mchanga na kushikishwa kisha kusemewa maneno ya kuomba msamaha kwa
kilichotokea.
Alisema walitakiwa waende na maziwa, unga wa mtama na hayo mavazi maalumu kwa ajili ya tambiko hilo.
Aliendelea kudadavua kwamba, kwa sasa Kanumba
hayupo duniani hivyo Wema anapaswa kuchukuliwa na kaka au mdogo wake wa
damu kwenda kutambika, ikiwa ni pamoja na kuzaa naye ili kufungua
mlango wa kizazi, hata kama ataachika basi ataendelea kupata watoto.
Baba Kanumba alisema mama mkubwa huyo ni
bibi yake mzee Charles Kanumba ambaye katika ukoo wao alikuwa mganga wa
wanawake walioshindwa kupata watoto au wenye tatizo la kizazi.
Hata hivyo, baba Kanumba alimalizia kwa kusema kuwa, ingekuwa zamani
ilikuwa ni kurithiwa tu lakini kwa sasa mila hizo zinapingwa
vikali.
Post a Comment