Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa maofisa wa Chama hicho Makao makuu, (jina linahifadhiwa kwa kuwa siyo msemaji), aliyetakiwa kutoa tathmini ya zoezi hilo kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, alisema wamepata malalamiko mengi kutoka kwa walioshindwa, wakilalamikia kukiukwa kwa kanuni, rushwa, upendeleo na wizi.
Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Pereira Silima
Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Pereira SilimaWAKATI kura za maoni zikileta shangwe na vilio kwa makada wa Chama Cha Mapinduzi kote nchini, watu walioangukia pua wakati wa kura za maoni wameshikana uchawi na wenzao wakiwatuhumu kuwa ndiyo chanzo cha anguko lao.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla
“Kuna malalamiko mengi na chama hakiwezi kukaa kimya, kitayafanyia kazi kwa kadiri inavyoweza ili washindi wawe wameshinda kwa haki, watakaokutwa na hatia kwa mujibu wa taratibu zetu, watashughulikiwa. Tunataka kuwahakikisha wana-CCM wote kuwa chama hakiwezi kufumbia macho tuhuma dhidi ya yeyote,” alisema ofisa huyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, mawaziri watano na wabunge wengi walikuwa wameanguka katika kura za maoni, miongoni mwao wakiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma, Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Pereira Silima na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma
Kuanguka kwa mawaziri na wabunge hao kumesababisha baadhi yao kuhama chama hicho kuelekea upinzani, huku wakitoa tuhuma mbalimbali zinazoonyesha kutoridhishwa kwao na matokeo ya kura hizo za maoni, ambazo hata hivyo, siyo muamuzi wa mwisho.
Post a Comment