PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jami.
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),amewataka wanachama wa chama hicho kukijenga kwa nafasi walizonazo iwe kiongozi au mwanachama wa kawaida.
Lipumba ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama waliofika katika ofisi ya makao makuu ya chama hicho wakitaka kauli ya yake juu ya chama na taarifa zilizopo katika mitandao juu ya kutaka kuachia nafasi yake uenyekiti wa chama hicho.
Lipumba amesema kuwa chama ni taasisi sio chama mtu mmoja anaweza kufanya kila kitu hivyo wanachama tambueni hivyo.
Aidha amewataka wanachama waisome katiba ya chama hicho kwa sababu zipo ili kuweza kujua chama jinsi kinavyoendeshwa kutokana na katiba ambayo inapitishwa na wanachama.
Wakati huo huo mkutano ulitishwa na chama hicho kwa lengo la Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa,Ibrahim Lipumba umearishwa kutokana na wazee wa chama hicho kuvamia Ofisi hiyo na kwenda kuzungumza na mwenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza wakati kuarisha Mkutano huo Mwenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu Bara,Magdalena Sakaya amesema kuwa mkutano huo ulikuwa wa mwenyekiti Lipumba lakini wazee wa chama wamevamia hivyo hawezi kuzungumza tena.
Sakaya amesema kitu ambacho alikuwa anataka kuzungumza anajua mwenyewe hivyo haiwezekani mtu mwingine azungumze kitu cha mwenyekiti.
“Jamani tunaahirisha mkutano wetu ambao ulitakiwa kuzungumzwa na mwenyekiti lakini wazee wa chama wamevamia ofisi na kuwa na mazungumzo na mwenyekiti”amesema Sakaya Naibu Katibu Mkuu Bara.
Post a Comment