Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kung'atua rasmi umwenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida wa chama hicho.
Lipumba amesema ataendelea kuwa mwanachama halali kwani kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020.Ameyasema hayo katika ukumbi wa mikutano wa Peacock hoteli jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti
wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa
kawaida kulia, Abdala Shabani pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji
wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza
na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha
CUFtaifa, Profesa Iblahimu Lipumba akitangaza kujiuzulu wadhifa
wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya
Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti
wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Rasimu ya
Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa ndio
iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi
(UKAWA) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli
ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti
wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua
uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mwenyekiti
wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha
yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha
CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es
Salaam leo.
Post a Comment