Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

YANGA SC VS AZAM FC, VITA YA NIYONZIMA, MIGI,

Capture
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Ame Ally, Kipre Tchetche na John Bocco wanataraji kuanza katika safu ya mashambulizi ya Azam FC wakati itakapo wavaa Yanga SC katika mchezo wa Robo fainali ya michuano inayoendelea ya Cecafa Kagame Cup 2015.

Timu hizo bora zaidi katika soka Tanzania Bara zitakutana kwa mara ya pili katika michuano hiyo. Mara ya mwisho zilikutana katika mchezo wa Fainali miaka mitatu iliyopita na Yanha walishinda kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali na kutwaa ubingwa wao wa Tano. MECHI YA LEO….. Azam FC haijaruhusu goli lolote huku ikiwa imeshinda michezo yote mitatu iliyopita na kufunga mabao Tisa, wakati wapinzani wao Yanha wanaingia katika mchezo wa leo wakitoka kushinda michezo mitatu ,mfululizo.

Yanga imepoteza mchezo mmoja kati ya minne iliyokwisha cheza katika hatua ya makundi. Ikiwa imetoka kundi gumu zaidi katika michuano ya mwaka huu, mabingwa hao mara mbili mfululizo wa zamani wangependa kuungana na Al Khartoom na Gor Mahia ambazo tayari zimefuzu kwa nusu fainali.

Timu hizo za Sudan Kaskazini na Kenya zilikuwa kundi A pamoja na Yanga. BOCCO, AME & KIPRE Walinzi wa Yanga watakutana na washambuaji wa ‘ daraja la juu Afrika Mashariki na Kati’.

Kipre tayari amefunga mabao Matatu katika gemu tatu zilizopita, wakati Bocco amefunga mara mbili. Nyota hao wawili wamekuwa wakiifunga Yanga mara kwa mara na wanaweza kufanya hivyo kwa mara nyingine Jumatano hii na kuipeleka timu yao nusu fainali. Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub na ‘ patna wake’ Kelvin Yondan walionekana kupata shida sana wakati walipokutana na GOR ambayo ilikuwa ikipanga na kufanya mashambulizi ya uhakika siku ya ufunguzi na walionekana ‘ kuteswa-kimtindo’ na kinara wa mabao katika michuano hii, nahodha wa Al Khartoum, Salh Eldin katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ambao walishinda 1-0.

Joseph Zuttah na Mwinyi Hajji wamecheza vizuri hadi sasa, walinzi haoo wa pembeni-Kulia na Kushoto watalazimika kucheza vizuri zaidi wakati watakapoikabili safu ya mashambulizi ya Azam FC.

Zuttah amekuwa akipandisha timu kwa mashambulizi ya uhakika akitokea upande wa kulia, Wakati Mwinyi amekuwa imara, mwepesi na mwenye pasi za uhakika katika beki mbili. Wawili hao ambao wamechukua nafasi za Juma Abdul na Oscar Joshua wameifanya safu ya ulinzi wa kati kuwa na utulivu.

Yanga watashambulia kama kawaida yao na watatumia zaidi sehemu za pembeni ili kufikisha mipira mbele kwa k uwa eneo la katikati ya uwanja linataraji kuwa ‘ gumu’ kupitisha mipira kutokana na aina ya wachezaji ambao watacheza sehemu hiyo.

Jean Mugiraneza, Salum Abubakary na Himid Mao wanaweza kuanzishwa kama viungo watatu wa Azam FC, wakati, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke wanaweza kuanza katika nafasi ya kiungo upande wa Yanga.

Azam wamekuwa wakitumia nguvu zaidi katika idara nyingi lakini wachezaji wao wa nafasi ya kiungo ni wagumu huku pia wakiwa na ufundi wa kumiliki mpira.

Niyonzima amekuwa akitawala sana mechi dhidi ya Azam FC na safari hii atakutana na nahodha msaidizi katika timu yake ya Taifa ya Rwanda, Mugiraneza. Tutaona mpira wa hali ya juu kama wachezaji hawatachezeana rafu za ubabe. TAMBWE, NGOMA & BUSUNGU, Washambuliaji hao watatu wataanza kwa pamoja katika safu ya mashambulizi ya Yanga. Tambwe amefunga magoli mawili, Busungu amefunga mara tatu wakati, Ngoma bado anatafuta goli lake la kwanza klabuni Yanga. Washambuliaji hao watatu wanaweza kufunga hata magoli mawili na zaidi katika gemu moja na kufanya hivyo mbele ya safu ya ulinzi ambayo haijaruhusu goli lolote katika gemu tatu mfululizo itakuwa ni jambo kubwa.

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris na Paschal Wawa wamekuwa wagumu kupitika, labda ni kutokana na aina ya timu walizokutana nazo lakini kiu-alisia, Yanga wanapaswa kupambana hasa ili kuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Azam katila michuano hii.

Safu yao ya mashambulizi imefunga magoli lakini bado wanakabiliwa na tatizo la upotezaji wa nafasi rahisi za kufunga magoli. Wawa amekuwa sababu kubwa ya ubora wa sasa katika safu ya ulinzi kutokana na uchezaji wake wa nguvu, uhamasishaji huku akiwa si mchezaji wa kufanya makosa yasiyotarajiwa.

Kapombe tayari amehusika katika magoli mawili ya timu yake. Mlinzi huyo wa kulia anaweza kuwa tatizo kwa Yanga kutokana na krosi-pasi zake, ni mchezaji asiyechoka kwenda mbele pale inapohitajika lakini uchezaji wake huo unaweza kuwa tatizo kwa kuwa, Ngoma si mchezaji wa kumuachia uhuru sana.

Nyoni ameendeleza kiwango chake kizuri na hivyo ataendelea kupangwa katika kikosi cha kwanza. Atamkabili, Kaseke ambaye amecheza kwa kiwango cha juu katika gemu nne zilizopita, wakati Wawa na Aggrey watakuwa macho kuhakikisha, Tambwe na Busungu hawapati nafasi ya kufunga. Nani mshindi wa gemu hii?. Ni mechi ngumu ila naipa Yanga asilimia 60 za kushinda kutokana na uzoefu wao wa michuano.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top