
Elizabeth Lauten ,ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano wa mbunge Stephen Fincher alitoa matamshi yake katika mtandao wa facebook ambayo baadaye yalifutwa.
Baada ya kukosolewa Bi Lauten aliomba msamaha kwa kutoa matamshi hayo ya kukera.
Aliku akikosoa sketi fupi zilizovaliwa na wasichana hao wa Obama.Bi Lauteni pia aliwashtumu wasichana hao kwa kuonyesha uchovu wakati waliposimama na baba yao katika sherehe hiyo ya ikulu ya Whitehouse.

''Kwa wapendwa Sasha na Malia: najua kwamba bado mko katika usichana wenu lakini ninyi ni miongoni mwa familia ya kwanza ya taifa hili, tafadhali jaribuni kuwa na heshima.Tafadhalini jaribu kuheshimu jukumu mlilopewa.
''Mama yenu na baba yenu hawaheshimu nyadhifa zao kama inavyohitajika na taifa kwa jumla.
Kwa hivyo naona kwamba mnakosa ile hadhi ya kuwa kioo cha jamii.
Maandishi hayo yaliendelea na kuwashauri wasichana hao kuonyesha kwamba wanaishi katika ikulu ya Whitehouse.
Vaeni mavazi ya kuonyesha mnahitaji kuheshimiwa sio kama mko katika baa.
Post a Comment