MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki
wa injili Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu katika shtaka
linalomkabili la ubakaji linalomkabili.
Katika shtaka hilo Mbasha anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) ambaye ni shemeji yake.
Mbele ya Hakimu Flora Mjaya, mwendesha Mashtaka Munde Kalombola alidai
mahakama imemkuta Mbasha na hatia baada ya kupitia ushahidi wa pande
zote mbili.
Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji maarufu wa muziki wa injili Flora
Mbasha anadaiwa kumbaka shemeji yake huyo kati ya Mei 23 na 25 mwaka huu
eneo la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo Septemba 5, 2013 ambapo
binti huyo aliieleza Mahakama kuwa alibakwa na shemeji yake (Mbasha) kwa
awamu mbili tofauti kabla ya kufanikiwa kukimbia.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2003 sura
ya 20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu, kesi hiyo inasikilizwa
na Mahakama ya siri ili kulinda haki ya binti huyo.
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Julai 23, mwaka huu ambapo
Mbasha anatakiwa kufika na mawakili wake ili kujitetea dhidi ya shtaka
hilo
Post a Comment