Unadhani Diamond anaamini uchawi >>> “Japokuwa vitabu vya dini vinasema ‘ndele’ zipo lakini haupaswi kuamini… Kuamini ni sawa na kumkiuka Mwenyezi MUNGU”>>>Kuna beef kati yake na Ali Kiba? Na vipi zile Team kwenye Mitandao ya Kijamii >>> “Sijawahi kuwa na beef nae hata siku moja… Sioni kama kuna ubaya wowote, kila mtu ana maamuzi kumchagua mtu anayemtaka yeye kumshabikia, huwezi kumlazimisha mtu” >>>
Kuna malipo ya collabo >>> “Sijawahi kufanya malipo kufanya nyimbo na mtu yoyote.. Mwanzoni ilikuwa tabu, sasahivi wanafahamu kwamba kufanya nyimbo na Diamond inakuwa rahisi nyimbo kufahamika East Africa… nimefanya collabo na karibuni wasanii wote wakubwa Africa.” >>>
Show ya MTV Road to MAMA Nigeria aliipataje? >>> “Ni mwaliko wa MTV, wa kwanza nilipewa South Africa nikafanya vizuri, wakaona wanipe na sehemu nyingine”>>>Diamond.
“Muziki wetu umekuwa na nafasi nzuri sana Africa, ni kazi kubwa sana imefanywa… Kuna utaratibu unaandaliwa kuona kama tutaweza kuwabeba watu kama mashabiki na Watangazaji..
Tupige kura kwa siku hata mara moja sio mbaya, kama tulichukua ‘Channel O’ sasa hivi tutashindwaje”
Nimeirekodi Interview yote, kama ulipitwa unaweza kuisikiliza hapa yote.
Post a Comment