Na Makongoro Oging’ MAAJABU!
Tajiri mmoja mkazi wa jijini Dar es Salaam, Walter Urio anayemiliki
biashara mbalimbali zikiwemo hoteli na baa, wiki iliyopita alikuta
maajabu ndani ya gari lake baada ya mtu kuingia ndani wakati milango na
madirisha yote yalikuwa yamefungwa, Uwazi linathibitisha.
Walter Urio meneja wa hoteli.
Tukio hilo la aina yake lilitokea nje ya Hoteli ya Nexus iliyopo
Makumbusho karibu na kituo cha mabasi ambapo mtu huyo, Shaban Alphan
alipopekuliwa, alikutwa akiwa na vitu vya ajabu kama ngozi ya fisi,
tunguri na hirizi
Mwandishi wa gazeti hili aliyefika eneo la
tukio mapema, alishuhudia umati mkubwa wa watu wakiwa wamelizunguka gari
hilo aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T732 BQV,
wakimlazimisha kushuka ili wampe kipigo, wakimtuhumu huenda ni
mshirikina aliyetumwa kummaliza tajiri huyo.
Kijana aliyekutwa kwenye gari.
Alipoulizwa sababu za kuingia katika gari hilo, Shaban alidai kuwa
alipanda akiamini ni basi la abiria lifanyalo safari zake kati ya
Makumbusho na Bagamoyo kwa vile alikuwa akielekea huko, lakini
akashindwa kufafanua jinsi alivyoingia wakati milango na madirisha ya
gari hilo yalikuwa yamefungwa.
Hata hivyo, tajiri huyo alifanikiwa kuwasihi wananchi hao kutochukua
sheria mkononi, badala yake aliwataka wamuache ili awaite polisi ambao
walikuja kumchukua baada ya kuwa amepelekwa katika ofisi ya mradi wa
kituo hicho cha mabasi.
Tunguri alizokutwa nazo.
Akisimulia ilivyokuwa, tajiri huyo alisema alikuwa amepitia sokoni
ili kununua baadhi ya bidhaa za hotelini na alipofika hapo, alifunga
milango yote na madirisha na kuendelea na mambo yake. Lakini
alipomwambia kijana wake akalifanyie usafi gari hilo, alishangaa baada
ya kuambiwa katika siti ya nyuma, kulikuwa na mtu.
Baada ya kwenda na kumhoji kijana huyo, mara watu walisogea na kutaka
kumuua, lakini wao, wakiongozwa na meneja wa hoteli hiyo, Godfrey Hamis
walifanikiwa kumuokoa kwa kuomba asipigwe badala yake afikishwe Kituo
cha Polisi Kijitonyama (Mabatini).
Gari alilokutwa.
Mwandishi wetu alifika katika kituo hicho cha polisi na kukuta Shaban
akiwa mahabusu na polisi wakathibitisha kuwa amefunguliwa jalada la
uchunguzi namba KJN/RB/24/2015.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;
Filed Under:
Updates
on Monday, 15 June 2015
Post a Comment