Timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) usiku wa leo inakabiliana na Misri katika mechi ya kuwania
kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) itayopigwa
kwenye uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria.
Mechi ya Stars inaanza majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Akiongelea mchezo wa leo kocha
wa Stars Mart Nooij amesema, anashukuru kikosi kimefika salama nchini
Misri na kipo katika hali nzuri, vijana wana ari na morali ya hali ya
juu, anaamini timu itafanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya wenyeji
Misri.
Nooij amesema mchezo wa leo ni
muhimu kwake, na kikosi chake kitacheza mpira wa kasi na pasi za haraka
haraka, huku safu ya ushambuliaji ikihakikisha inatumia vizuri nafasi
itakazozipata.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mh. Juma Nkamia naye yupo jijini Alexandria kwa
ajili ya kuipa sapoti Taifa Stars.
Post a Comment