Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mbunge wa
Ukonga Eugen Mwaiposa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3,
2015.
Waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wameshiriki kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga
Eugen Mwaiposa aliyefariki dunia juzi.
Shughuli ya kuaga mwili wa mbunge huyo ilifanyika jana mchana nyumbani
kwa mbunge huyo maeneo ya Chadulu mjini Dodoma, na kuhudhuriwa pia na
viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini na serikali akiwemo mkuu wa
mkoa wa Dodoma, Kepteni mstaafu Chiku Galawa.
Katika salamu zake Naibu Spika wa bunge Mh. Job Ndugai kwa niaba ya
Bunge, aliuelezea msiba kuwa ni pigo kwa bunge na taifa kiujumla, kwa
kuwa mambo mengi mazuri aliyokuwa nayo marehemu bado yalikuwa
yanahitajika.
Kwa upande wao baadhi ya wabunge waliohudhuria shughuli hiyo kwa
uwakilishi wa makundi yao walisema watamkumbuka marehemu kwa mengi ikiwa
ni pamoja na uwezo wake wa kusimamia hoja mbalimbali za maendeleo
katika jimbo lake.
Baada ya shughuli ya kuaga, mwili wa marehemu Mwaiposa ulisafirishwa
kutoka Dodoma kwa njia ya Ndege na uliwasili alasiri nyumbani kipunguni
Dar es salaam.
Mwili wa Mwaposa utazikwa jijini Dares salaam katika eneo la Kipunguni siku ya Jumamosi.
Post a Comment