Mshambuliaji mpya wa Yanga SC Malimi Busungu leo asubuhi ametupia nyavuni goli mbili wakati timu yake ikipata ushindi wa goli 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Friends Rangers mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume uliopo maeneo ya Ilala kwenye ofisi za (TFF), Dar es Salaam.
Kpah Sherman alikuwa wakwanza kuipatia Yanga goli la kwanza akimalizia pasi safi kutoka kwa Busungu na kuiweka Yanga mbele kwa goli 1-0. Lakini Mussa Juma aliisawazishia Rangers goli hilo dakika ya 25 ya mchezo.
Busungu aliifungia Yanga bao la pili akitumia vizuri pasi aliyogongewa na Sherman na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko huku Yanga wakiwa mbele kwa goli 2-1.
Kipindi cha pili Rangers walifunga goli la pili kupitia kwa Cosmas Lewis goli hilo likiwa ni la kusawazisha lakini muda mfupi kabla mchezo haujamalizika, Busungu alitupia kambani bao la tatu na la ushindi na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3-2
Post a Comment