Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ameanza
vibaya ziara yake wilayani Sengrema, Mwanza baada ya wananchi kumzomea.
Tukio hilo limetokea jana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Zeno uliyopo Sengerema mjini, Mwanza.
Katika mkutano huo, Nape alizungumza maneno yaliyowatibuwa wananchi hasa wale wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa UKAWA.
Kwenye
kauli zake Nape ambaye yupo katika ziara moja na Kinana aliwaambia
wananchi hao kuwa, baadhi ya vijana wamekuwa wakipewa viroba ili wafanye
fujo.
Nape
aliwalaumu vijana hao kwamba, wanapewa pombe aina ya viroba na viongozi
wa vyama vya upinzania ili kwenda kufanya fujo katika mikutano ya chama
hicho tawala.
“Chadema
kimechoka sasa hivi lakini nyie vijana bado mmeng’ang’ani tu, mnapewa
viroba na vikisha panda mnashikilia bendera ya ‘Peoples Power’ bila
kufahamu kwamba, chama chenu kimeisha poteza mwelekeo.
“Kuna
watu wanasema eti CCM ifungashe vilago vyake katika Wilaya ya Sengerema
kwa kuwa Chadema inaingia katika uchaguzi huu, hicho kitu
hakitawezekana na wao ndio wataondoka, mtang’ang’ania sana,” amesema
Nnauye.
Kauli hiyo iliyosababisha baadhi ya wafuasi wa Chadema kuanza kuzomea na hata kusababisha mkutano huo kusimama kwa saa moja.
Hata
hivyo, Kinana hakuweza kuvumilia hali hiyo na kuamka kutoka sehemu
aliyokuwa amekaa na kumfuata Nape kumwambia ashuke kutoka jukwaani na
kutumia nafasi hiyo kuwaomba radhi wananchi hao.
Katika
hatua hiyo, Kinana alitumia nafasi hiyo kuwaweka sawa wananchi hao kuwa
CCM ipo imara na haitetereke kwa chochote na kwamba, itatumia kanuni na
misingi ya chama hicho katika kuijenga nchi na kuleta maendeleo.
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimekuwa na nguvu kubwa
Post a Comment