Muigizaji wa filamu, Shamsa Ford amesema tangu aachane na aliyekuwa mume wake Dickson Matoke, amewahi kuwatishia kuwaua yeye na mwanae zaidi ya mara 10.
Shamsa alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV kuwa ex wake huyo alikuwa na matatizo mengi ambayo alishindwa kuyavumilia.
“Namshukuru baada ya kuwa gizani sasa hivi nipo kwenye mwanga.
Dickson kanifanya nijifunze vitu vingi sana, vitu vingi vya kifamilia
nilikuwa nafanya mimi kama mimi, yeye kazi yake ni kukesha baa anakunywa
pombe na marafiki zake.Nimeshagombana na marafiki zake wote,” Shamsa
alimwambia mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema.
“Kuhusu kumtaka mtoto huo ndo ugomvi wetu huwa tunagombana kila siku.
Sababu ya kwanza kwanini namnyima mtoto wangu Dickson alishaonyesha
roho mbaya kwa mtoto wangu na mwanamke yoyote ambaye una uchungu na
mtoto wake huwezi kumuachia mtoto.
"Dickson alitamka sio mara moja, siyo
chini ya mara kumi, katamka kwangu, mbele ya ndugu zake , katamka kwa
marafiki zangu kwamba ‘ipo siku nitakuja kumuua Shamsa na mtoto wake.’
"Hilo neno zito sana, yule mtu yupo desperate, hana kitu chochote cha
kupoteza. Leo hii ninaweza nikampa mtoto akaona ‘huyu Shamsa huyu
anaringa acha nimkomoe,’ akimuua mtoto wangu halafu yeye akaenda Segerea
hana cha kupoteza, lakini mimi nitaumia sana.” aliongeza kwa uchungu.
Katika hatua nyingine Shamsa amekanusha kutoka kimapenzi na Nay wa Mitego na kudai kuwa bado hajafikiria kurudi kwenye uhusiano.
Post a Comment