
Makundi hasimu ya wanajeshi yanakabiliana katikati ya mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya DW mchana huu, rais Nkurunzinza ametoa tamko fupi kupitia ukurasa wa twitter wa rais akiwataka wananchi wa Burundi kuwa watulivu.
Taarifa ya DW pia imearifu kuwa Mkuu wa majeshi nchini Burundi Meja Jenerali Prime Niyongabo ametangaza kuwa jaribio hilo limefeli.
Hata hivyo,Mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi ya Burundi Meja Jenerali Godefroid Niyombare ambaye ndiye aliyeongoza mapinduzi hayo amesema kuwa hizo ni propaganda tu za baadhi ya wanajeshi watiifu kwa rais Nkurunzinza.
Niyombare amesema kuwa kama ni kweli mapinduzi yamefeli, basi rais Nkurunzinza arudi nchini leo,asiporudi leo basi hakuna haja ya kubishana juu ya uwepo wa mapinduzi hayo.
Post a Comment