Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa katika pozi na miss huyo.
Chanzo cha ‘unyunyuzi’ huo kilitonya kwamba, mlimbwende huyo amekuwa
akionekana mara kwa mara akijivinjari na Diamond jambo ambalo wadau
wamelishtukia na kubaini kuwa ana mpango wa kuingilia penzi la Zari na
kusambaratishia uchumba wa wawili hao.Ijumaa Wikienda lilinyetishiwa habari hizo hivi karibuni na kuamua kuzifanyia kazi hatua kwa hatua, ambapo liliweza kujiridhisha kwa baadhi ya matukio ya picha ambazo mrembo huyo amekuwa akipiga na Diamond.
Ukiachilia mbali uchunguzi huo, mwanahabari wetu alimtafuta mrembo huyo kwa lengo la kutaka kujiridhisha juu ya madai hayo ambapo alikiri kuwa na ukaribu na Diamond huku akifafanua kwamba uhusiano wake na jamaa huyo si wa kimapenzi kama wengi wanavyomchukulia.
“Hizo picha za karibu zaidi ni zile ambazo tulipiga kwenye bethidei ya meneja wa Diamond aitwaye Salaam, ambayo ilifanyika pale nyumbani kwake (Salaam) Kijitonyama (Dar) hivi karibuni.
“Ni kweli watu wengi wananituhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond lakini si kweli maana ninajuana naye kawaida tu,” alisema Glory.
Kwa upande wa Diamond aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa ni kweli anamfahamu Glory ila si mpenzi wake na anachokijua ni shabiki wake kama ilivyo kwa wengine.
Alisema hata picha alizopiga naye hakuna picha za hovyo maana zilipigwa hadharani.
“Glory ni shabiki wangu wa kawaida tu kama ilivyo kwa mashabiki wangu wengine, suala la kupiga naye picha halimaanishi ni demu wangu,” alisema Diamond.
Post a Comment